HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 11, 2022

PSPTB YATOA TAARIFA YA UPATIKANAJI WA HUDUMA KATIKA OFISI ZAKE


Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetoa taarifa kwa umma kuwa kwa sasa huduma zake zote bado zinapatikana katika ofisi za Bodi hiyo zilizopo jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza wakati wa kutoa taarifa hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred B. Mbanyi amesema kuwa huduma za upatikanaji wa vyeti vya uanachama zitaendelea kutolewa ofisi ya Dar es salaam mpaka siku ya Mahafali ya 11 ya mitihani ya Kitaaluma ya PSPTB yatakayofanyika tarehe 15 Oktoba 2022, ambapo huduma hiyo itahamishiwa rasmi katika ofisi za PSPTB Dodoma.

Mbanyi amesema kuwa PSPTB inaendelea kusisitiza kuwa wale wote wanaohitaji vyeti vyao kupitia ofisi ya Dar Es Salaam wajitahidi kuvifuata kabla ya mahafali ili kuepuka usumbufu wa kuvifuata Dodoma.

Pia amewasisitiza na kuwakumbusha wanaohitaji huduma nyingine zote kuwa zitaendelea kupatikana ofisi zote za PSPTB yaani ofisi ya Dar Es Salaam na Dodoma na Ofisi za Dodoma zimeanza kufanya kazi toka tareh 30 Mwezi wa 09, 2022 katika jingo la Mkandarasi Place ghorofa ya Saba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Godfred B. Mbanyi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad