*Amesema
NSSF kupitia uwekezaji wa mradi wa Mzizima Tower inadhihirisha kuwa
inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika
suala zima la uwekezaji wenye tija
Na MWANDISHI WETU
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Mhe. Profesa Joyce Ndalichako amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Mhe.
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kufungua
fursa mbalimbali zikiwemo za uwekezaji hapa nchini.
Mhe. Profesa
Ndalichako amesema hayo leo tarehe 22 Oktoba, 2022 jijini Dar es
Salaam, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi
wa jengo la kitega uchumi la Mzizima Tower linalomilikiwa na Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
“Tunafahamu namna ambavyo Mhe.
Rais wetu Samia Suluhu Hassan anafungua fursa za Uwekezaji, kwa hiyo
nanyie NSSF mnatengeneza mazingira ambayo wawekezaji watakapokuja nchini
watapata sehemu ya kuishi na sehemu ya kufanya biashara zao,” amesema
Mhe.Profesa Ndalichako.
Mhe. Profesa Ndalichako amesema kupitia
uwekezaji huo wa mradi wa Mzizima Tower inadhihirisha kuwa NSSF inaunga
mkono juhudi ambazo zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan.
Amesema kukamilika kwa
mradi huo kutaendana na kazi kubwa ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan
amekuwa anaifanya ya kufungua uchumi wa nchi, kuweka mazingira mazuri
kwenye sekta binafsi na kukaribisha wawekezaji nchini.
“Tumeshuhudia
kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambavyo
imefungua fursa na hivi sasa wawekezaji kutoka Mataifa mbalimbali
wanakuja nchini, hivyo bado tunahitaji majengo mengi zaidi ya biashara
ikiwemo hoteli ya namna hii,” amesema.
Amewasihi NSSF kuendelea
kufanya kazi kwa wakati ili Serikali iweze kuona manufaa ya mradi huu,
pia na fedha za wanachama ambazo zimewekezwa kupitia mradi huu zianze
kurejeshwa, lakini kubwa zaidi mtengeneze ajira kwa vijana ambapo mradi
huo ukianza kufanya kazi ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa
moja zinaweza kufika 1000.
Mhe. Profesa Ndalichako pia amepongeza
Bodi ya Wadhamini, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba na
Managementi kwa kazi kubwa mnayofanya hasa ya kuondoa changamoto
mbalimbali zilizokuwa zimejitokeza katika mradi huu ambao
utakapokamilika utachagiza maendeleo ya Taifa na wananchi kwa jumla.
Naye, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema maendeleo ya ujenzi wa mradi huu yanaendelea vizuri.
Kwa
upande wake, Msanifu wa Majengo ya Mzizima Tower, Kaisi Kalambo
amemueleza Mhe. Waziri Profesa Ndalichako kuwa maendeleo ya mradi huo
yamefikia asilimia 88 na kuwa jengo hilo likikamilika litatumika kwa
matumizi ya ofisi, hoteli na makazi.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, (hayupo pichani), mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea mradi wa uwekezaji wa jengo la Mzizima Tower jijini Dar es Salaam, ambalo linamilikiwa na NSSF.
Msanifu Majengo, Kaisi Kalambo, akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, (hayupo pichani) kuhusu maendeleo ya mradi wa uwekezaji wa jengo la Mzizima Tower jijini Dar es Salaam,w ambalo linamilikiwa na NSSF.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, akiendelea kukagua maeneo mbalimbali katika mradi wa uwekezaji wa jengo la Mzizima Tower, jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa
mradi wa uwekezaji wa jengo la Mzizima Tower lililopo jijini Dar es
Salaam, linalomilikiwa na NSSF.
Matukio katika picha
No comments:
Post a Comment