Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Ndejembi amewaasa wananchi kuacha tabia ya kutumia fedha za mkopo unaotokana na dhamana ya hatimiliki ardhi kuolea mke wa pili na kwenda mjini kutumbua raha.
"Mkitumia fedha hizo za mkopo zikaisha, taasisi za fedha mlikokopa zitakuja kutaifisha mashamba yenu,"Ndejembi.
Ndejembi ametoa onyo hilo alipokuwa akihutubia baada ya kuzindua jengo la masijala lililojengwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) katika Kijiji cha Nakalonji, Kata ya Mbondo wilayani Nachingwea Oktoba 12, 2022.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Naibu Waziri Ndejembi akiwaasa wananchi kuhusu matumizi ya mkopo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA

MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO TV/BLOG
0754264203
No comments:
Post a Comment