HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 3, 2022

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NJE CZECH AWASILI NCHINI KWA ZIARA

 


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa amewasili nchi leo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 2 hadi 4 Oktoba 2022.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Tlapa amepokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme na Balozi wa Tanzania nchi Ujerumani ambaye pia anawakilisha Jamhuri ya Czech, Mhe. Dkt. Abdallah Possi.

Akiwa nchini, Mhe. Tlapa kwa nyakati tofauti, atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Nchi-Tamisemi, Waziri wa Afya, Waziri wa Viwanda na Biashara, pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) pamoja na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Hospitali ya Jeshi la Wananchi (JWTZ).

Tanzania na Czech zimekuwa zikishirikiana katika sekta za elimu,utamaduni, afya, biashara na uwekezaji.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa amewasili nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Tanzania nchi Ujerumani ambaye pia anawakilisha Jamhuri ya Czech, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa walipokuwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Czech, Mhe. Martin Tlapa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad