MWENYEKITI WA CCM WILAYA KIBAHA AMEZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUTOA HUDUMA STAHIKI KWA WANANCHI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 21, 2022

MWENYEKITI WA CCM WILAYA KIBAHA AMEZITAKA TAASISI ZA SERIKALI KUTOA HUDUMA STAHIKI KWA WANANCHI

Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Kibaha Mjini Mwilimu Mwajuma Nyamka akizungumza katika kikao maalumu cha Halmashauri Kuu kimepokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mkuu wa CCM 2020-2025 kwa kipindi cha Januari – Juni 2022.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha Mji Mhandisi Mshamu Munde katika kikao maalumu cha Halmashauri Kuu kimepokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mkuu wa CCM 2020-2025 kwa kipindi cha Januari – Juni 2022.
Baadhi ya wanachama Wa CCM wakiwa kwenye kikao hicho.

Na Khadija Kalili, KIBAHA
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mji Mwl. Mwajuma A. Nyamka ameongoza kikao cha Halmashauri kuu maalum ya CCM Wilaya ya Kibaha Mjini amezitaka Taasisi za serikali kutoa huduma stahiki na zenye tija kwa wananchi wa Kibaha Mji.

Nyamka amesema hayo kwenye kikao kilichokaa Jumatano tarehe 19/10/2022, kikao hicho maalumu cha Halmashauri Kuu kimepokea, kujadili na kupitisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mkuu wa CCM 2020-2025 kwa kipindi cha Januari – Juni 2022.

Halmshauri Kuu imepokea taarifa za taasisi wezeshi kutoka TANROAD, DAWASA na TANESCO .

Aidha Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Kibaha imeelekeza Kamati ya Siasa Wilaya kufanya ziara ya kutembelea Viwanda vilivyopo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Kibaha ili kuweza kujionea jinsi wawekezaji wanavyoendesha kazi zao za kila siku na kuangalia maslahi ya wafanyakazi mahusiano ya wawekezaji na jamii inayoizunguka.

Pamoja na mambo mengine Halmashauri Kuu kwa kauli moja imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, kwa namna anavyoendelea kuiongoza vizuri serikali ya awamu ya sita na kutafsiri kwa vitendo

utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mkuu CCM mwaka 2020-2025 katika kuimarisha huduma za kijamii, kuimarisha ustawi wa wananchi, kukuza uchumi wa nchi na wananchi wa wilaya ya kibaha na Tanzania nzima kwa ujumla.

Wakati huohui Halmashauri Kuu imempongeza Mbuge wa Jimbo la Kibaha Mjini Mheshimiwa Slyvestry Koka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mheshimiwa Mussa Ndomba na Waheshimiwa Madiwani wote wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwa jinsi wanavyoshirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanavyoshirikiana na serikali kuchagiza maendeleo, maslahi na huduma muhimu za wananchi wa Kibaha.

Kwa namna ya pekee Halmashauri kuu imempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mhandisi Mshamu Munde kwa jinsi anavyojituma kufanya kazi kwa bidii na uzalendo hasa kwa kitendo alichofanya kwenye machinjio ya pangani mtaa wa mtakuja kwa kuvua suti na kuvaa nguo za ufundi kwaajili ya kushilikiana na mafundi umeme kwa vitendo mpaka akagundua tatizo la umeme mdogo lilikuwa linasumbua mradi mtambo kutofanya kazi vizuri kwa muda wa mwaka kasoro, sasa mafundi wapo kazini kuhakikisha umeme unafika haraka.

Katibu Uenezi na Siasa Wilaya ya Kibaha Mjini Clemence Kagaruki amesema kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Kibaha Mjini imepokea taarifa ya fedha za tozo kiasi cha Mil. 760 na kuridhishwa na na mpangilio mgawanyo wa matumizi ya fedha hizo katika Halmashauri ya Mji wa Kibaha huku wataalamu wakisisitizwa wasimamie fedha za wananchi vizuri kama ilivyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad