MERIDIANBET SOKA BONANZA NI NURU KWA VIPAJI VYA VIJANA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 30, 2022

MERIDIANBET SOKA BONANZA NI NURU KWA VIPAJI VYA VIJANA

 

MERIDIANBET Soka Bonanza wiki hii lilikuwa pale maeneo ya Yombo Kiwalani, kwenye ule uwanja wenye historia kubwa ya matukio ya kimichezo, na timu nzima kutoka Meridianbet iliandika historia nyingine ya kuwapa burudani ya msimu wakazi wa maeneo hayo kwa Soka safi na Zawadi za kutosha kama Jezi, Mipira, Soksi na Glovu na zawadi nyingi.

Ilikuwa ni kama ndoto kwa vijana wa maeneo yale ambao walikuwa wakiwaza ni nani atakaewashika mkono, kwenye kupambania vipaji vyao na hatimaye ndoto yao ikatimia pale ambapo Meridianbet walipoamua kuwashika mkono kwa kufanikisha jitihada zao za kufika mbali.

Timu nne kutoka maeneo tofauti ya Jiji la Dar Es Salaam haswa maeneo hayo ya Yombo Kiwalani zilikutana na kutunishiana misuli, sio wengine ni Ajax FC, Kiwalani United na Kiwalani FC, pamoja na Kigilagila FC palikuwa hapatoshi. Meridianbet walidhihirisha Ukubwa wao kwa kuzikutanisha timu hizi pamoja na waamuzi bora kabisa kama mahakimu wa mchezo huo.

Mara baada ya bingwa kupatikana wachezaji na makocha hawakuwa nyuma kutoa shukrani zao kwa kampuni ya michezo ya kubashiri Tanzania na Afrika Mashariki ya Meridianbet, kwani waligusa mahitaji yao muhimu ya kimichezo hususani vifaa.

Timu ya Kiwalani United iliibuka mshindi wa fainali za Meridianbet Soka Bonanza zilizofanyika siku ya jumamosi ya tarehe 29/10/2022, kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kiwalani, kwa mikwaju ya penati 5-4 ambapo mchezo ulienda mpaka kipindi cha pili bila mshindi kupatikana, ikabidi mshindi apatikane kwa mikwaju ya penati. Meridianbet wanaendesha Kasino mtandaoni na michezo mingi ya kubashiri, jiunge na jumba la mabingwa sasa.

Mshindi wa Kwanza alipata zawadi ya Kikombe na Seti moja ya Jezi kamili, mipira miwili, soksi pea 3, glovu 1 na kitambaa cha unahodha. Na mshindi wa pili alipata zawadi ya Jezi Seti moja kamili, mipira miwili, soksi pea moja, glovu na kitambaa cha unahodha.

Mchezo wa kwanza ulichezwa kati ya Ajax FC dhidi ya Kiwalani United mchezo uliojaa ufundi mkubwa na wachezaji wengi wenye vipaji, lakini mpaka dakika 90 hakupatikana mbabe.

Baada ya Dakika 90, ilibidi kanuni zifuatwe kwa kutumia mikwaju ya penati ndipo mshindi aliyeenda kucheza fainali alipatikana, Ajax FC walitolewa kwa mikwaju ya penati, 5-3.

Mechi ya pili ilikuwa ni kati ya Kiwalani Boys dhidi ya Kigilagila FC ambao kwa asilimia kubwa ilikuwa na vijana wengi wanaochipukia, wakati Kiwalani Boys wakitumia udhaifu wa Kigilagila FC na kuwafunga magoli 2-0 na hivyo kuwalazimisha kucheza mechi ya mshindi wa tatu.

Mshindi wa 3, alikuwa ni timu ya Ajax FC ambapo walipata Zawadi ya seti moja kamili ya jezi, mpira mmoja, soksi 1, glovu ya mlinda mlango 1 na kitambaa cha unahodha kimoja.

Meridianbet ni wakongwe wa kuendesha michezo ya kubashiri Tanzania, wakiwa na ofa kubwa, odds bora na machaguo mengi zaidi Tanzania. Wanakupa nafasi ya kufurahia ushindi kuanzia kwenye michezo yako pendwa na maarufu hadi Odds Kubwa za kasino na Jackpots mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad