HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 26, 2022

M-BET yaingia mkataba wa miaka mitano na Simba Queens wenye thamani ya Sh1 billion

 
Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-BET imeinga mkataba wa miaka mitano na klabu ya Simba Queens wenye thamani ya Sh bilioni 1.

Simba Queens kwa sasa wapo mjini Rabat, Morocco ikishiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mkurugenzi wa masoko wa M-BET Tanzania Allen Mushi alisema kuwa wameamua kuingia mkataba na timu hiyo kutokana na mafanikio makubwa ya wa timu hiyo kwenye ligi kuu ya wanawake Tanzania na katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Cecafa.

Mushi alisema kuwa klabu hiyo itakuwa inapata Sh Million 200 kila mwaka pamoja na mahitaji mengine muhimu ikiwa mishahara, bonasi na mambo mengine.

Alisema kuwa mafanikio ya Simba Queens yanafahamika na kila kampuni itataka kuingia nayo mkataba kutokana na mafanikio hayo.

“Tunajisikia faraja kubwa kuidhamini Simba Queens baada ya mkataba mnono wa billion 26.1 tuliongia na timu ya wanaume. Mpaka sasa, kila mpenda soka anajua mafanikio ya klabu ya Simba kwa soka la Afrika na tunajivunia kuingia mkataba na timu ya wanawake,” alisema Mushi.

Alisema kuwa anaamini kuwa siku moja Tanzania itatwaa ubingwa wa dunia kupitia soka la wanawake.

“Kuna mwamko mkubwa wa soka la wanawake mpaka sasa, msukumo uliopo sasa, umetufanya kuingia na hamasa kubwa na kuendelea kuchangia maendeleo ya michezo hapa nchini,” alisema’

Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez aliipongeza kampuni ya M-Bet Tanzania kwa kuingia mkataba huo wa kihistoria kwa timu za wanawake hapa nchini na kuongeza kuwa watahakikisha wanafanya vyema katika mashindano ya Afrika na ligi ya hapa nyumbani ambayo ni mabingwa watetezi.

Gonzalez alisema kuwa udhamini wa mkataba huo hautahusiana na ule wa wanaume ambao walioingia kwa timu kubwa ya Simba wanaume mwezi Agosti mwaka huu.

Alisema kuwa awali, walifanya mazungumzo na makampuni mbalimbali lakini M- Bet imeonyesha dhamira ya kuhitaji kusaidia na kuinyanyua soka la wanawake kupitia Simba Queens.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Katikati) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh1 billioni kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez (kulia). Kushoto ni Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Katikati) akizungumza wakati wa kutangaza udhamini wa miaka mitano ya udhamni wa klabu ya Simba Queens wenye thamani ya sh bilioni 1. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez na kulia ni Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Katikati) akionyesha jezi ambazo klabu ya Simba Queens itazitumia katika mechi zake baada ya kusaini mkatana wa miaka mitano wenye thamani ya Sh 1 billioni. Kulia ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez na kushoto ni Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad