Kampuni
 ya uuzaji na unganishaji wa magari na mitambo ya Gf Trucks & 
Equipment’s Ltd imeibuka kuwa kampuni ya kwanza inayouza na kusambaza 
Magari na mitambo ukanda wa mikoa ya kanda ya ziwa.
Hayo 
yamejiidhihirisha wakati wa kufunga maonesho ya 5 ya teknolojia ya 
madini mkoani Geita na kuibuka kampuni bora ya usambazaji na uuzaji wa 
mitambo.
 Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na 
Waziri wa Viwanda na uwekezaji Ashatu Kijaji,Afisa masoko na mauzo wa 
kampuni ya GF Poul Msuku alisema wanafurahia kuibuka washindi katika 
kipengele hicho na wanachukua tuzo hiyo kama chachu ya kujipanga na 
kuongeza nguvu kaitia uwekezaji kwa kanda ya ziwa.
Gf Trucks 
ambao ni wauzaji wa mitambo na mashine za migodini aina ya XCMG, na 
magari ya kubebea mizigo ya FAW na Hongyang wana wateja wengi 
wanaojihusisha na Uchimbaji wa madini na shughuli za usafirishaji 
nchini,
Pia Gf waliitumia siku ya kufunga maonesho kwa kukabidhi 
Mtambo wa kuchimbia madini kwa mteja aliyenunua katika maonesho hayo ya 
madini kwa bei ya punguzo.
 Pia Waziri Kijaji aliwataka Gf 
kuwekeza zaidi katika kwawezesha wachimbaji wadogowadogo ili waweze 
kujikomboa na kwa kuwawekea utaratibu rahisi kumudu gharama, ikiwemo 
mikopo rahisi na pia aliwataka wachimbaji hao kuchapa kazi itakayoweza 
kumwongezea kipato na kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.
 
Nae 
Mkuurugenzi wa kampuni ya G Unity Squre Ltd,Ezekiel Rembo aliwashukuru 
GF kwani kwa kushiriki katika maonesho hayo, wameweza kununua mashine 
hiyo (XCMG) kwa gharama nafuu tofauti kama wangeifuata Dar essalaam na 
kwamba ameokoa zaidi ya shilling million 10 ikiwamo gharama ya mafuta 
kuitoa Dar hadi Geita alimaliza .
Waziri wa Viwanda na uwekezaji, Ashatu Kijaji akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa kwanza kwa makampuni yanayouza na kusambaza Magari na mitambo Migodini Afisa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Gf Trucks & Equipments Ltd ,Poul Msuku wakati wa kufunga maonesho ya Madini mkoani Geita.
Waziri wa viwanda na uwekezaji Ashatu Kijaji akimkabidhi funguo ya mtambo wa kuchimbia Madini (Excavator ) ya XCMG Mkurugenzi wa kampuni ya G Unity ,Ezekiel Rembo baada ya kununua katika maonyesho ya madini kwa punguzo malum mkoani Geita
Mkurugenzi wa E Unity akiangalia mtambo wa Excavator baada ya kukabidhiwa katika viwanja vya maonyesho
 

 
 



 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment