Doris Mollel ashiriki Mkutano wa Pumzi ya Maisha - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 3, 2022

Doris Mollel ashiriki Mkutano wa Pumzi ya Maisha

Muanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji  Taasisi ya Doris Mollel ambaye pia ni Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel akizungumza katika Mkutano uliopewa jina la "Pumzi ya Maisha" (The Breath of Life) uliojadili namna ya Kuongeza Upatikanaji wa Oksijeni Endelevu, ulioandaliwa na Taasisi ya FREO2 yenye makao makuu yake nchini Australia. Doris Mollel, alielezea ni kwa namna gani Taasisi yake imekuwa ikishirikiana na serikali karika kusaidia watoto njiti hasa kwa kuchangia vifaa tiba na kushauri namna ambayo huduma za mama na mtoto zinaweza kuboreshwa nchini Tanzania. Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Igongo, ilichopo mjini Mbarara, nchini Uganda.
Muanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji  Taasisi ya Doris Mollel ambaye pia ni Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (mwenye koti la kijani) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wengine wa Mkutano huo, uliojadili namna ya Kuongeza Upatikanaji wa Oksijeni Endelevu, ulioandaliwa na Taasisi ya FREO2 yenye makao makuu yake nchini Australia.
 
Muanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji  Taasisi ya Doris Mollel  (kushoto) akimsikiliza Muanzilishi mwenza wa Taasisi ya Freo2, Bryan Sobbort alipokuwa akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo, uliojadili namna ya Kuongeza Upatikanaji wa Oksijeni Endelevu, ulifanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Igongo, ilichopo mjini Mbarara, nchini Uganda. 
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad