Mkuu
wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Melvin Saprapasen (
wa tano kushoto), Meneja wa Absa Tawi la Ohio, Ally Janja (kushoto
kwake), wafanyakazi wa Absa pamoja na Wateja wakigonganisha glasi
kutakiana afya njema na mafanikio katika moja ya matukio kuadhimisha
Wiki ya Huduma kwa Wateja ya benki hiyo jijini Dar es Salaam wiki
iliyopita. Katika maadhimisho hayo viongozi wa ngazi za juu wa benki
hiyo walitembelea matawi ya Absa nchini kote ili kuzungumza na
wafanyakazi na pia Wateja wao ili kuweza kuona namna bora ya kuwahudumia
na kushughulikia mahitaji yao.
Wafanyakazi
wa Benki ya Absa Tawi la Alpha House pamoja na Wateja wao wakitakiana
afya njema na mafanikio katika hafla iliyoandaliwa na tawi hilo kwa
wateja wao, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Mkuu
wa Mtandao wa Matawi wa Benki ya Absa Tanzania, John Beja (katikati,
mwenye tai nyekundu) Mkurugenzi wa Fedha wa Absa Tanzania, Obedi Laiser
(nyuma ya Beja), wakiselebuka pamoja na wafanyakazi na wateja wa Tawi la
Absa Mikocheni, kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja tawini hapo,
jijini Dar es Salaam wiki iliyopita
Meneja
wa Benki ya Absa Tawi la Zanzibar, Rabia Abood (katikati), akikabidhi
zawadi kwa mmoja wa wateja wake, Jabir Alfarsy katika hafla kuadhimisha
Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi hilo visiwani humo hivi karibuni.
Kushoto ni Meneja wa wateja Maalum katika tawi hi
lo, Salim Salum.
Meneja
wa Benki ya Absa Tawi la Pugu, Heri Sijaona (kushoto), akizungumza na
wateja wa benki hiyo tawini hapo jijini Dar es Salaam hivi karibuni,
katika hafla ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Meneja
wa Benki ya Absa Tawi la Slipway, Veronica Okio (kulia), akikabidhi
zawadi kwa mmoja wa wateja wake katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa
Wateja, tawini hapo, Dar es Salaam hivi karibuni.
Meneja
wa Kitengo cha Bima wa Benki ya Absa Tanzania, Sandeep Chavda
(kushoto), akimpa zawadi mmoja wa Wateja wa Absa Tawi la Dar City, huku
Meneja wa tawi Hilo, Winford Mwang'onda akiangalia, katika hafla ya
kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja tawini hapo, Dar es Salaam hivi
karibuni
Mmoja
wa watumishi waliofanyakazi kwa muda mrefu katika Benki ya Absa Tawi la
Tanga, Mwanajumaa Darweshi (wa pili kulia), akionesha cheti cha
shukurani muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja
Binafsi wa Absa Tanzania, Ndabu Lilian Swere (kushoto), katika hafla
iliyofanyika pamoja na maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika
tawi hilo, mjini Tanga juma lililopita. Wa pili kushoto ni Meneja wa
tawi hilo, Gloria Mallya.
No comments:
Post a Comment