Vodacom Tanzania Foundation imetoa msaada wa vifaatiba vya vyenye thamani ya zaidi ya 130 milioni kwa hospitali za wilaya ya Kilindi na Handeni - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 21, 2022

Vodacom Tanzania Foundation imetoa msaada wa vifaatiba vya vyenye thamani ya zaidi ya 130 milioni kwa hospitali za wilaya ya Kilindi na Handeni

 

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel (katikati) akipokea baadhi ya vifaa vya kuhudumia watoto njiti vyenye thamani ya shilingi 110 milioni viliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa wilaya mbili za Handeni na Kilindi, ili kuendeleza juhudi za kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati nchini. Wa pili kushoto ni mkuu wa wilaya ya Handeni Siriel Mchembe aliyepokea vifaa hivyo mwishoni mwa wiki.

=======

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation leo imekabidhi vifaatiba vya watoto wachanga na uzazi katika hospitali za wilaya ya Kilindi na Handeni mkoa wa Tanga ili kusaidia afya ya kinamama na watoto mkoani humo.

Hospitali za wilaya ya Handeni na Kilindi zinahudumia takribani wanawake 2,600 kwa mwaka ambapo kati ya hao, wanawake 91 hujifungua kabla ya wakati. Msaada huu wa vifaatiba unalenga kuhudumia watoto njiti 300 kwa mwaka huku ukitoa msaada pia kwa wilaya jirani.

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation Bi. Rosalynn Mworia alisema “Tunafuraha kuwepo hapa mkoani Tanga kutoa msaada huu muhimu ili kusaidia mipango ya afya ya uzazi kwa kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 110 milioni vitakavyosaidia kuokoa maisha ya watoto njiti wanaozaliwa mkoani hapa. Msaada huu umeambatana na michango ya wafanyakazi wa Vodacom kupitia mpango wetu wa “Pamoja na Vodacom” ambapo wafanyakazi wa Vodacom hujitolea kusaidia jamii inayowazunguka na leo hii wametoa kwa ajili ya manunuzi ya vifaa vya kusaidi akina mama nawatoto wachanga.”

Vodacom Tanzania Foundation imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo mashine za kuongeza oksijeni, vitanda vya joto, mashine za kupima mapigo ya moyo, mashine za ultrasound na vinginevyo vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi 110 milioni kwa hospitali mbili za wilaya hizo.

Takwimu zinaonyesha kwamba kila mwaka watoto 15 milioni huzaliwa kabla ya wakati yaani njiti, kusini mwa jangwa la sahara ikiwemo Tanzania ambapo watoto 1 milioni hufariki kwa kukosa huduma muhimu. Kwa zaidi ya miaka kumi taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia vifaa tiba katika vituo vya afya na hopsitali  hapa nchini ili kuokoa maisha ya watoto njiti.

“Watoto njiti wana nafasi kubwa ya kukua na kuwa na afya nzuri bila ulemavu endapo watapata msaada wa vifaa na usimamizi wa afya kuzingatiwa na ndio maana tunaendelea kutoa msaada ili kuokoa maisha ya watoto  njiti.  Mpaka sasa katika juhudi zetu za kupunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga tumefikia mikoa 12 nchini Tanzania.  Tunafuraha kutoa msaada kwenye huduma ya afya ya uzazi nchini kwa sababu hili ni eneo tunalohisi ni muhimu kwa maslahi ya taifa letu.” Aliongeza. 

Akipokea vifaa hivyo Mhe. Dk Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya alitoa shukrani zake kwa Vodacom Tanzania Foundation akisema kwamba msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa mkoa huo kufikia malengo yake ya afya ya watoto wachanga pamoja na wajawazito.

“Msaada huu umekuja muda muafaka ambapo serikali inashinikiza kupunguza vifo vya watoto wachanga na wajawazito. Vodacom imekuwa ikiongoza kwa kutumia teknolojia na mtandao wake kusaidia juhudi za serikali na hivi karibuni tumetambulisha huduma ya m-mama katika mkoa huu. Hivyo tunaamini tutafikia lengo letu hivi karibuni” alisema.

Kwa upande wake, Jonathan Bedenu mganga mkuu wa mkoa wa Tanga alisema “Tunafuraha kupokea msaada huu na tunaimani utasaida watoa huduma kuokoa maisha ya watoto njiti na kuwapa nafasi ya kuishi maisha bora. Tutahakikisha kuwa vifaa vinatunzwa vizuri ili viweze kuhudumia watu wengi na kwa muda mrefu zaidi”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad