Wakati mbio za NMB Marathon
zikitarajiwa kutimua vumbi Septemba 24 mwaka huu, klabu ya NMB Jogging
yenyewe jana Jumatatu ilianza kujifua mapema kwa ajili ya kujiweka
tayari kushiriki mbio hizo.
Jogging hiyo ilianza kujiandaa na
mbio hizo kushirikiana klabu ya EFM Jogging ambapo walianza maandalizi
hayo kwa kukimbia mbio za kilomita nane. Mbio hizo zilianzia kwenye
Ofisi za NMB, Posta jijini Dar.
Mbio hizo za NMB Marathon ambazo
huu ni msimu wake wa pili zinatarajiwa kurindima katika Viwanja vya
Leaders, Dar ambapo mgeni wake rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mhe.
Kassim Majaliwa.
Mbio hizo zenye kauli mbiu ya Mwendo wa Upendo
zinafanyika maalum kwa ajili ya kuchangisha fedha kusaidia matibabu ya
akina mama wenye matatizo ya Fistula.
Meneja wa NMB Jogging,
Stella Motto amesema wana siku chache kabla ya kufikia Septemba 24
ambapo NMB Marathon itafanyika, hivyo wameona wapashe misuli ili wawe
sawa na kuwakumbusha wadau kujisajili na mbio hizo zenye lengo kuu la
kukusanya fedha kwa ajili ya kina mama wenye matatizo ya fistula.
Kwa
upande wake mwakilishi wa EFM, Tunu Hassan alisema “Hii siyo mara ya
kwanza kwa NMB kurudisha kwa jamii, hivyo nasi tumeona tuungane nao kwa
ajili ya jambo hilo.
Jisajili na NMB Marathon kupitia https://marathon.nmbbank.co.tz/
au sogea Mlimani City kila Jumasosi na Jumapili kuanzia saa 3 asubuhi
mpaka 12 jioni. Pia, Mtana Bar(Oysterbay) na Juliana Pub( Mbezi Beach)
Ijumaa, jumamosi na jumapili kuanzia saa 6:30 mchana mpaka saa 4 usiku.
Wanachama
wa klabu za jogging kutoka NMB na EFM wakipasha misuli katika Makao
Makuu wa Benki ya NMB, jijini Dar es salaam kabla ya kuanza mazoezi ya
kukimbia pamoja ikiwa ni maandalizi ya Mbio za hisani za NMB Marathon
zenye kauli mbiu ya “Mwendo wa Upendo” zitakazofanyika tarehe 24
Septemba 2022 – Leaders Club.
Wanachama wa klabu za jogging kutoka NMB na EFM wakiwa katika mazoezi
ya pamoja ikiwa ni maandalizi ya Mbio za hisani za NMB Marathon zenye
kauli mbiu ya “Mwendo wa Upendo” zitakazofanyika tarehe 24 Septemba
mwaka huu kuanzia viwanja vya Leaders club na kumalizikia katika viwanja
hivyo.
Tuesday, September 6, 2022

NMB Jogging mguu sawa 'Mwendo wa Upendo'
Tags
# HABARI MICHEZO
HABARI MICHEZO
Labels:
HABARI MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment