NBAA KUADHIMISHA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWAKE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 1, 2022

NBAA KUADHIMISHA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWAKE

 Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA) ni taasisi iliyopo chini ya Wizara yenye Dhamana ya Fedha na ilianzishwa kwa sheria ya Bunge Mwezi Novemba mwaka 1972 mpaka sasa mwaka 2022 inatimiza miaka 50. Bodi hii ilianza majukumu yake rasmi mwaka 1973.

Akizungumza wakati wa mahojiano, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema Bodi hiyo ilianzishwa kutokana na uhaba wa Wahasibu uliokuwepo kutokana na ukuaji mkubwa wa idadi ya mashirika ya umma, idara za Serikali na asasi mbalimbali za sekta Binafsi na pia gharama kubwa ya kuelimisha wahasibu wazalendo nje ya nchi ili kukidhi mahitaji yaliyokuweo kipindi hicho pamoja na kuwepo kwa mifumo tofauti ya utayarishaji na utafsiri wa Taarifa za Fedha.

Akizungungumzia Majukumu ya Bodi hiyo Maneno amesema kuwa jukumu la kwanza ni kusajili Wahasibu na Wakaguzi, jukumu la pili ni kusimamia taaluma ya Uhasibu. Jukumu la tatu ni Kutunga viwango vya uandaaji wa vitabu vya fedha na jukumu la nne ni kuendeleza taaluma ya Uhasibu.

Pia amesema katika kuendeleza taaluma ya Uhasibu nchini kuna majukumu mengine ambayo ni kutoa mitihani ya wahasibu na Wakaguzi wa hesabu kwa ngazi ya Utunzaji wa Vitabu vya Hesabu, Wahasubu wale wanaokwenda kusoma CPA na jukumu lingine ni kuishauri Serikali katika masuala yote yanayohusiana na masuala ya Fedha, Uhasibu na Ukaguzi.

" Tumeanza maadhimisho ya miaka 50 tangu Agosti, 2022 na tunategemea kufanya kilele cha maadhimisho hayo tarehe 30, Novemba 2022. Mambo mbalimbali yanafanyika kwenye maadhimisho hayo ikiwemo; kufanya mikutano na makongamano, kufanya shughuli za kijamii ikiwa ni kurudisha kwa jamii, kufanya mikutano na wanafunzi pamoja na wanaofundisha wanafunzi wanaotegemea kufanya mitihani ya Bodi" alisema Maneno
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad