HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 2, 2022

Muuza duka ashinda mamilioni ya M-BET

 
Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Mkazi wa Dar es Salaam Raphael Daudi amejishindia kitita cha Sh 113,789, 620 baada ya kubashiri kiusahihi mechi 12 za mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet Tanzania.

Daudi ambaye ni muuza duka eneo la Ubungo Riverside na shabiki wa Simba alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa yeye kushinda kiasi kikubwa cha fedha hicho kutokana na ugumu wa kubashiri kwa baadhi ya timu zilizokuwa zinacheza.

Alisema kuwa mchezo kati ya Crystal Palace dhidi ya Brentford FC ulimpa ugumu sana kubashiri kwa uharaka kutokana na matokeo ya timu zote mbili kabla ya mchezo huo.

“Mchezo huo ulikuwa mgumu sana kwangu kutabiri kutokana na matokeo ya awali, nilishindwa kubashiri haraka na baada ya kufikiria sana, nilibashiri matokeo ya sare na ndivyo ilivyokuwa,”alisema Daudi.

Daudi ambaye pia ni shabiki wa klabu ya Simba alisema kuwa atazitumia fedha hizo kwa kuongeza mtaji katika biashara zake na nyingine kujiendeleza kimasomo.

Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema Daudi anakuwa mshindi wa nane wa mwaka huu kuibuka mshindi katika jackpot ya PERFECT 12 tokea kuanza kwa mwaka huu.

Mushi pia aliwaomba Watanzania wenye umri zaidi ya miaka 18 kuendelea kubashiri kupitia M-BET ili waweze kubadili maisha na kushinda mamilioni ya fedha.

Mkuu wa Kitengo Cha Wateja Binafsi wa Benki CRDB, Stephen Adili alimpongeza Daudi kwa kushinda kiasi kikubwa cha fedha na kumshauri kutumia kiasi hicho cha fedha kuwekeza.

“Nampongeza Daudi kwa ushindi huu mkubwa na kikubwa zaidi ni mteja wa benki yetu yenye ushirikiano mkubwa na kampuni ya M-Bet Tanzania. Nawaomba vijana wenye umri kuanzia miaka 18 kubashiri na M-BET na vile vile kuweka fedha zao katika benki yetu na kuweza kushiriki katika promosheni yetu maarufu ya kuelekea kombe la dunia nchini Qatar,” alisema Adili.

Mkurugenzi  wa Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (kushoto) na  Mkuu wa Kitengo Cha Wateja Binafsi wa Benki CRDB, Stephen Adili (kulia) wakimkabidhi mfano wa hundi Raphael Daudi baada ya kushinda kitita cha Sh 113,789, 620  kwa kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet Tanzania.

Mkurugenzi  wa Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (kushoto) na  Mkuu wa Kitengo Cha Wateja Binafsi wa Benki CRDB, Stephen Adili (kulia) wakimkabidhi fedha Sh 113,789, 620  kwa kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet Tanzania.


Mshindi wa fedha taslimu Sh 113,789,620 wa mchezo wa kubashiri wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet Tanzania Raphael Daudi akipozi na mfano wa hundi baada ya kukabidhiwa jana. Daudi alishinda fedha hizo kwa kubashiri kwa usahihi mechi 12 za ligi mbalimbali duniani.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad