MAFANIKIO YA NBAA NDANI YA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWAKE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 5, 2022

MAFANIKIO YA NBAA NDANI YA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWAKE

 

Katika miaka 50 ya Bodi, NBAA imefanya mambo mengi makubwa. Idadi ya watahiniwa na waliofahulu mitihani ya Bodi imeongezeka na kufikia takribani elfu 26,286 na kati ya hao elfu 11, 616 wamefaulu kwenye ngazi ya CPA na 14,408 katika ngazi ya ya Utunzaji wa Vitabu vya Hesabu. Vilevile kumekuwa na ongezeko la Makampuni ya Ukaguzi na utengenezaji wa Hesabu za Fedha yapatayo 450.

Akisema hayo leo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno, kwamba mwaka jana wamefanya makongamano 17 na bado yanaendelea kwa ajili ya wanachama wao na pia makongamano mengine wakishirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bima. Vilevile tumeweza kuandaa warsha na kongamano mbalimbali kila mwaka za kitaifa na kimataifa

"Tumeweza kutunga viwango vya kuandaa nakutayarisha hesabu za fedha katika sekta za Umma na Binafsi na vilevile tumetunga kanuni za uadilifu au maadili kwa wanachama wa Bodi." Alisema Maneno"Katika kipindi cha miaka 50 ya Bodi (1972 – 2022), Sheria ya Usajili wa Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu imerekebishwa mara mbili kwa Sheria (ya Marekebisho) Na. 2 ya 1995 na sura 286 ya mwaka 2002. Mwaka 2021 sheria hii ilifanyiwa marekebisho makubwa yaliyolenga pamoja na mambo mengine kuongeza ufanisi katika taaluma kwa kuhakikisha kuwa sharia, viwango na miongozo mbalimbali inazingatiwa kwa umakini zaidi ili kupunguza upotoshaji kathika kuandaa na utoaji wa taarifa za fedha nchini" alisema Maneno

Pia Bodi imefanikiwa kuweka vigezo vya utoaji wa misamaha (Exemption Criteria) kwa baadhi ya masomo yanayofundishwa na vyuo vya uhasibu nchini kwa wahitimu wa vyuo hivyo wanaotaka kuandika mitihani ya Bodi

Baada ya kuanzishwa kwake Bodi imeendelea kufanya jitihada kubwa katika kujenga na kudumisha ushirikiano na mahusiano mazuri na taasisi za taaluma ya uhasibu za kikanda na kimataifa ambapo mwaka 1973 ilishirikiana na taasisi mbalimbali duniani ili kuweza kubuni silabi, mitaala na mfumo wa mitihani ya taaluma ya Uhasibu ya kutumika Tanzania.

Ushirikiano huo ulijumuisha kuzitembelea taasisi husika na zenyewe kuitembelea Bodi ili kubadilishana ujuzi na uzoefu katika masuala ya usimamizi wa taaluma ya uhasibu na utungaji wa silabi, mitaala na mifumo ya mitihani ambazo ni CA ya England & Wales, ACCA (UK), CIMA (UK), CA (India), CA Pakistan, ICAW India, CPA America na CA (Sri Lanka).
Pia amesema, ndani ya Miaka 50 NBAA imeweza kujenga Kituo cha mikutano cha wanachama wetu yaani Accountancy Professional Center (APC) Bunju ambacho kina kumbi za mikutano mbalimbali ambazo kwa ujumla wanaweza kukaa watu elfu 3,000 pia kuna hoteli yenye vyumba zaidi ya 100.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA), CPA Pius A. Maneno


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad