MADEREVA WA MASAFA MAREFU, JAMII KUNUFAIKA NA MRADI WA HUDUMA ZA UKIMWI MKOANI PWANI-DKT.HEDWIGA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 13, 2022

MADEREVA WA MASAFA MAREFU, JAMII KUNUFAIKA NA MRADI WA HUDUMA ZA UKIMWI MKOANI PWANI-DKT.HEDWIGA

 Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

MADEREVA na Wasaidizi wao wanaokwenda masafa marefu kupitia mkoa wa Pwani kwenda nchi jirani Zambia na Malawi ,watanufaika na fursa ya huduma za Ukimwi zinazotolewa kituo cha afya Mkoani, Mlandizi, Chalinze na Mdaula ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU.

Jamii pia inakwenda kunufaika na huduma hizo ikiwa ni sanjali na kupima Ukimwi,kupata tiba, ushauri nasaha na kupata kondom.

Kamisheni ambayo ni bodi inayosimamia Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ,imefanya ziara kukagua mradi wa huduma za Ukimwi zilizopo mkoani Pwani, kandokando ya barabara Kuu Itokayo Dar es Salaam, Zambia Malawi ambapo ni sehemu ya mradi mkubwa wa uboreshaji barabara kuanzia Bandari ya Dar es Salaam,Tunduma,Mbeya hadi Mpaka wa Malawi.


Mwenyekiti wa Kamisheni TACAIDS dkt.Hedwiga Swai alisema, wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo ambapo katika kituo Cha afya Chalinze kilichojengwa na TACAIDS ,kimefikia asilimia 90 kukamilika na wananchi wanaendelea kupata huduma,elimu na kondomu.Hata hivyo Hedwiga alieleza,, walikuwa wakipata taarifa ya hatua ya vituo vinavyoendelea kwenye ripoti lakini baada ya kutembelea wamejiridhisha na ubora uliopo ."Majengo yamejengwa kwa ubora ukiacha vitu vidogovidogo,tukiangalia majengo yapo katika ubora wake, "Nilikuwa nasoma kwenye ripoti,"


"Pia kuna kondomu dispenser ,"zile imagination nikajua ni mashine fulani imekaa pale, dispenser, siunajua ni ya kubonyeza nikajua unabonyeza kinaanguka,nikaambiwa ni kitu kinakaa kondomu 400 ,anachukua tu suala ambalo ni zuri"alielezea Hedwiga.


Nae Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na tathmini TACAIDS Makao Makuu ,Jerome Kamwela alieleza , katika Mradi wa huduma za Ukimwi zilizopo mkoani Pwani wanapata bahati vituo vitano kufanyiwa ukarabati na kujengewa maabara, kupima Ukimwi,vituo vya tiba, sehemu ya kuchomea taka na kupata kondomu.


Alitaja vituo hivyo ni pamoja na Kituo Cha afya Mkoani, Mlandizi, Chalinze,Mdaula cha Maarifa na Zahanati ya Mdaula.


"Madereva Kama mnavyowajua na wasaidizi wao wana point wanazozitumia kupumzika usiku ,wakifika mfano hapa Chalinze wanaweza kupata dawa kwa wale wanaotumia dawa za kufubaza makali ya VVU, kondomu,elimu nasaha na huduma za Ukimwi zote."alifafanua Kamwela.


Awali mratibu wa Ukimwi Mkoani Pwani,Josephat Fransis alielezea ,kwasasa kiwango cha Ukimwi kipo kwa watu 46,264 ikiwa ni sawa na asilimia 5.5.


"Kiwango hiki ni cha tafiti za mwaka 2017, kwasasa utafiti mpya unafanyika na tathmini na kiwango kipya kitatolewa mwaka 2023,na tunaamini kwa mkoa kitashuka kutokana na juhudi tunazofanya dhidi ya maambukizi mapya na utoaji elimu."alisisitiza dkt.Josephat.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad