Dough Works Limited, Oryx Energies wazindua mgahawa Morroco jijini Dar - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 17, 2022

Dough Works Limited, Oryx Energies wazindua mgahawa Morroco jijini Dar

 


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Dough Works Limited, Vikram Desai akizungumza wakati wa uzinduzi wa mgahawa wa KFC katika kituo cha mafuta cha Oryx kilichopo Morroco jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wafanyakazi na wateja wakiwa katika uzinduzi wa mgahawa wa KFC katika kituo cha mafuta cha Oryx kilichopo Morroco jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Mgahawa wa KFC katika kituo cha mafuta cha Oryx kilichopo Morroco jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Dough Works Limited kwa kushirikiana na Oryx Energies Tanzania Limited washirikiana katika kufanya biashara hapa nchini.

 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Septemba 16, 2022 amesema kuwa wapo katika

jitihada za kuendelea kusambaza chakula chenye ubora wa hali ya juu na zenye matumizi rahisi zaidi ya mlaji (Mtumiaji).

Amesema Kampuni ya Dough Works Limited na Oryx Energies Tanzania Limited wamezindua Mgahawa wa KFC- Thru na BAO Café katika Kituo cha Huduma ya mafuta katika kituo cha Oryx Morocco.

Amesema Kampuni ya Dough Works Limited,ni ya kwanza nchini kupanua huduma za Migahawa ambazo zitakuwa Huduma ya Haraka kwani Ni wamiliki wa KFC & Pizza Hut nchini Tanzania pamoja na chapa yao inayokua kwa kasi ya BAO Café wanafuraha kwa kufungua mgahawa wao wa saba wa KFC na Mgahawa wa BAO ambao utakuwa wa 4 nchini Tanzania. KFC Drive-Thru iliyopo katika kituo cha ORYX Morocco utakuwa mgahawa mwingine baada ya migahawa iliyopo Mlimani City Mall, Masaki, Diamond Plaza - City Center, Mikocheni Plaza, Kariakoo na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Pamoja na ufunguzi wa migahawa mipya ya KFC, kampuni mpya ya Dough Works na BAO afé wanajivunia ushirikiano wa kukuza migahawa ya Kitanzania ili kufikia viwango vya Kimataifa za kutoa huduma zenye ubora na huduma ya kiwango cha kimataifa. Katika muda wa miezi mitatu tu, BAO Café imeona ukuaji wa haraka na jumla ya maduka 4 yamekua kwa kasi na mipango inaendelea kufungua maduka 2 zaidi kabla ya Mwaka 2022.

Kampuni ya Oryx Energies Tanzania Limited, sehemu ya Oryx Energies Group, inayotoa huduma ya Nishati inaonyesha dhamira yake ya dhati kutoa huduma rafiki kwa wateja wengi zaidi ili kukidhi mahitaji ya watu wanaohamia katika mtandao wake wa vituo vya huduma unaokua kwa kasi nchini.

Ufunguzi wa maduka 2 mapya kwa ushirikiano na Oryx Energies Tanzania Limited ni sehemu ya mpango mkubwa wa upanuzi wa chapa za Dough Works. Sambamba na mkakati wao wa ukuaji wa kujenga uhusiano na ushirikiano wanaotoa huduma za chakula ambazo ni rejareja, ushirikiano huu wa hivi karibuni na Oryx Energies Tanzania Limited utaruhusu kuweka maduka yajayo katika maeneo muhimu kote nchini, na kufanya huduma kupatikana kwa urahisi zaidi na kutaongeza thamani na huduma itapatikana kwa urahisi zaidi na kwa watanzania wote.

Desai, meeleze shauku yake kwa uzinduzi wa ushirikiano huo akisema, “Leo tunasherehekea uzinduzi wa ushirikiano huu mzuri na wa kimkakati kati ya Dough Works Limited na Oryx Energies Tanzania Limited. Pamoja na ufunguzi wa duka letu katika Kituo cha Oryx Morocco, tunaendelea kutimiza ahadi yetu ya kutoa chakula chenye ubora wa juu na Kinachopatikana kwa urahisi nchini Tanzania. KFC ni chapa ya kimataifa, yenye maduka 23,000 yaliyopo katika nchi zaidi ya 140 duniani kote. Tunayofuraha kusambaza huduma hii ya chakula yenye migahawa mashuhuri duniani kote na kutoa nafasi kwa watumiaji kupata huduma bora. Tunayofuraha zaidi kuzindua chapa mpya kabisa ya BAO Café, ambayo imeundwa na kuendelezwa kwa njia ya kipekee ili kutoa huduma kwa urahisi katika maeneo muhimu ili kukidhi mahitaji ya watumiaji. Tunatarajia kufanya ufunguzi wa eneo huduma yetu hapa ORYX Morocco, tunafurahi kuwa na ushirikiano wa kibiashara na Mshirika ambaye ni hodari katika ubunifu ambaye ni Oryx Energies Tanzania Limited.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania, Kalpesh Mehta, amesema, “Mahitaji ya bidhaa za nishati yanaongezeka mwaka hadi mwaka nchini Tanzania na Oryx Energies inapanua shughuli zake kwa kutoa mapendekezo mapya na viwango vipya vya huduma ya Nishati, Ufunguzi wa Mgahawa huu mpya wa KFC Drive-Thru na BAO Cafe katika eneo letu la ORYX Moroco unaashiria nia njema ya kutoa huduma bora kwa wadau wetu.

Vituo vyetu vya vinavyotoa huduma ya Nishati vinatoa ofa mbalimbali za jumla na rejareja kwa wateja wetu, zaidi ya utoaji wa huduma ya mafuta,pia tunatoa huduma ya vilainishi na LPG pamoja na huduma za ziada kama vile kuosha magari. Tunafuraha kufanya kazi na mshirika aliyejidhatiti na aliyethabiti katika kampuni yake ya Dough Works Limited., kuhusu hili tukio letu na katika miradi ya upanuzi ya siku zijazo nchini Tanzania Kati ya KFC, BAO Café & Pizza Hut, jumla ya maduka 23 huhudumia maelfu ya watu na kutoa huduma ya chakula cha mchana na chakula cha jioni kila siku, na huduma hii ni rafiki na rahisi kwa watumiaji na ikiwa imedhamiria kukidhi mahitaji ya soko.

“Kwa kufunguliwa kwa KFC Drive-Thru na BAO Café katika Kituo cha Huduma cha Oryx Morocco, watumiaji sasa wanaweza kutembelea hapa na kupata huduma bora ambayo itakuwa rafiki kwa wote.”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad