HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 22, 2022

DIT WAASWA KUANGALIA UNAFUU KATIKA MRADI WA UFUNGAJI MIFUMO YA GESI KWENYE MAGARI

 

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa akisikiliza Maelezo kutoka kwa Mhadhiri wa Tasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam (DIT),Dk John Msumba juu ya namna gari linalotumia gesi asilia linavyofanya kazi wakati wa Maonesho ya Mkutano wa 19 wa Bodi ya usajili wa Wahandisi Nchini(ERB) Katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion Center Dodoma.
Waziri wa Ujenzi na UchukuziProf. Makame Mbarawa, akisikiliza Maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano Kutoka Tasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT), Amani Kakana.

Na Humphrey shao, Michuzi Tv
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa ameitaka Tasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Kuangalia namna itakavyo leta unafuu katika mradi wa ufungaji mfumo wa gesi kwa magari hapa Nchini.


Waziri Mbarawa amesema hayo mapema leo Septemba 22, 2022 jiji Dodoma wakati alipotembelea Maonyesho katika Mkutano wa 19 Bodi ya Usajili wa Wahandisi Nchini uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention center.


"Hii ni teknolojia nzuri na itatusaidia sana kupambanana hizi changamoto lakini tuangalie namna ya kuweza kupunguza gharama za ufungaji." Amesema Waziri Mbarawa.


Amesema kuwa ukiachilia mbali kupunguza Bei Tasisi hiyo inapaswa kufanya mchakato wa haraka kuyafikia magari yanayotumia Dizeli hili nayo yaweze kufaidika na gesi asilia.


Waziri Mbarawa amefungua milango kwa DIT kufika kumuona kwa ushauri kwani licha ya yeye kuwa Waziri lakini amechapisha maandiko manne yanayohusu teknolojia ya gesi asilia katika matumizi ya magari.


Kwa upande wake Mhadhiri kutoka DIT, Dk. John Msumba amemuhakikishia Waziri kuwa Tasisi yake inafanya kila namna ufungaji huo wa gesi uwe kwa bei nafuu lakini changamoto kubwa wanayokutana nayo ni Kodi ya vipuri wanavyoingiza kutoka nje.


"DIT inatamani kufunga vifaa hivyo bei nafuu kwa utumiaji wa gesi ni Rafiki wa mazingira lakini changamoto kubwa ni wanapoingiza vifaa hivyo Bandarini kwani mpaka Sasa avijapatiwa msamaha wa Kodi." Amesema Dk. Msumba.


Amemaliza kwa kuishukuru serikali na Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Samia Suluhi Hassan kwa kuendelea kuishika mkono tasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad