HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 1, 2022

DKT JAFO AFUNGUA MKUTANO WA MABADILIKO YA TABIANCHI

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akifungua Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo leo Septemba 1, 2022 jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, mkutano ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Uingereza na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akitoa neno la utangulizi wakati Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo leo Septemba 1, 2022 jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Uingereza na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar akizungumza wakati wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo leo Septemba 1, 2022 jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Uingereza na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo leo Septemba 1, 2022 jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Uingereza na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiteta Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar akizungumza wakati wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo leo Septemba 1, 2022 jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Uingereza na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ametoa wito kwa mataifa duniani kushirikiana katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Ametoa wito huo leo wakati akifungua Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi na Maendeleo uliofanyikajijini Dar es Salaam leo Septemba Mosi, 2022 ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano na Serikali ya Uingereza na kushirikisha zaidi ya nchi 20 duniani.

Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Dkt. Jafo alisema Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingi duniani inakabaliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alisema changamoto hizo zinaathitri uzalishaji wa chakula unaosababishwa na ukame na mafuriko ya kudumu, uharibifu wa miundombinu, uharibifu wa ardhi, uchakavu wa vyanzo vya maji, upotevu wa maji. ya viumbe hai, viumbe vamizi, uhamiaji na mlipuko wa magonjwa.

Hivyo, Waziri Jafo alisema kutokana na athari hizo, Tanzania inatumia wastani wa Dola za Kimarekani milioni 500 kwa mwaka katika kuchukua hatua za kukabiliana na hali hiyo.

“Katika Mkutano tutaweza kujadiliana na wenzetu kutoka mataifa mbalimbali duniani kuhusu changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na namna ya kupata fedha za zitakazotumika katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi,” alisema.

Aidha, Dk. Jafo alibainisha kuwa Tanzania iliazimia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kati ya asilimia 30 hadi 35 ikilinganishwa na mazingira ya Biashara ya hewa ya ukaa ifikapo mwaka 2030, ambapo takriban tani milioni 138 hadi 153 za hewa hiyo zinatarajiwa kupungua.


Kwa upande wake Balozi wa Uingereza Mhe. David Concar alisema Mkutano huo ni jukwaa muhimu la kuzikutanisha nchi mbalimbali kujadili namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mhe. Concar alisema kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kuwa nchi zinazoendelea kuchangia katika mapambano hya mabadiliko ya tabianchi katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP26) uliofanyika Glasgow, Scotland ni wakati sasa wa kutekeleza maazimio hayo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Dkt. Omar Dadi Shajak alisema maeneo 143 ya Visiwia vya Zanzibar yameathiriwa na mabadiliko ya tabianchi kwa kuingiliwa na majichumvi kutoka baharini.

Alisema kutokana na changamoto hiyo kilimo cha mpunga kimeathiriwa na athari za mabadiliko ya tabianchi hali iliyosababisha uzalishaji wa mpunga kupungua kwa kiasi kikubwa.

Hivyo, Dkt. Shajak alisema Mkutano huo utasaidia kuweka mikakati endelevu ikiwemo kutafuta njia mbadala wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad