HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 28, 2022

Class atamba 'kumkalisha' Mmexico Mlimani City.

 
Bondia nyota wa Tanzania Ibrahim Class ametamba kumchapa mpinzani wake Gustavo Pina Melgar kutoka Mexico katika pambano la kimataifa lililopangwa kufanyika Ijumaa (Septemba 30) kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Pambano hilo limeandaliwa na kampuni ya MO Boxing, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo chini ya mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji.

Class alisema kuwa baada ya kukaa nje ya ulingo kwa muda mrefu, ameamua kurejea kwa kasi kwa lengo la kutwaa mikanda mbalimbali ya ngumi za kulipwa nchini.’

Alisema kuwaamejiandaa vyema kwa ajili ya pambano hilo na hatamdharau mpinzani wake kwani anaamini naye amekuja kwa ajili ya ushindi. “Najua Melgar ni bondia mzuri lakini si kwa kufikia kwangu, nimejiandaa vyema na nimuonyesha jinsi gani Tanzania ina mabondia wazuri na wenye vipaji vikubwa,” alisema Class. Kwa upande wake, Melgar alisema kuwa amekuja kusaka ushindi ili kuboresha rekodi yake katika ngumi za kulipwa.

Mratibu wa pambano hilo kutoka MO boxing Ahmed Seddiqi alisema kuwa maandalizi yamekamilika na ambapo kutakuwa na mapambano sita ya utangulizi.

Pambano la kwanza la utangulizi litakuwa kati ya bondia nyota wa Ghana, Alfred Lamptey ambaye atapambana na bondia Abraham Ndauendapo kutoka Namibia huku Juma Choki akizichapa na bondia wa kutoka Mexico Jose Hernandez ambapo bondia kutoka Kenya Nicholas Mwangi atapimana ubavu na Emmanuel Mwakyembe wa Tanzania.

Pambano lingine litakuwa baina ya bondia Sameer Anwar dhidi ya Adam Mrisho huku Mwinyi Mzengelaakizichapana Sabari J na pambano lingine litakuwa baina ya Lulu Kayage dhidi ya Sadra Mohamed.

Pambano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Azam TV, Boxer, MO XTRA, Mlimani City, KCB Bank, White Sands Resorts, Bajaj na OTAPP. Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa benki ya KCB, Christine Mnyenye alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kudhamini mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.

“Tunajisikia fahari kubwa kudhamini mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini ikiwa si mara etu ya kwanza, tutatumia mchezo huu kutambulisha huduma yetu ya mpya ya bima na kuwaomba wadau wa ngumi za kulipwa na watu wengine kujiunga nayo ili kujiwekea kinga na majanga mbalimbali,”alisema Mnyenye.



Mratibu wa pambano la kwanza la kampuni ya MO Boxing Ahmed Seddiqi (Katikati) akiwatambulisha mabondia Ibrahim Class wa Tanzania (kushoto) na Gustavo Pina Melgar wa Mexico ambao watapambana Ijumaa kwenye ukumbi wa Mlimani City
Mratibu wa kampuni ya MO Boxing Ahmed Seddiqi (katikati) akiwatambulisha mabondia Ibrahim Class (watatu kushoto) na Gustavo Pina Melgar wa Mexico (wa tatu kulia) kuelekea pambano la Ijumaa (Septemba 30) kwenye ukumbi wa Mlimani City. Wa kwanza kushoto ni Fauqiya Shareer wa benki ya KCB akifuatiwa na Ashish Josh wa Bajaj ambapo wa kwanza kulia ni Salim Salim wa JustFit na Mkii wa Masoko na Uhusiano wa benki ya KCB Christine Manyenye.


. Mratibu wa pambano la kwanza la kampuni ya MO Boxing Ahmed Seddiqi (Katikati) akizungumza katika mkutano wa kuwatambulisha mabondia ambao watapambana Ijumaa kwenye ukumbi wa Mlimani City
Ibrahim Class (kushoto) na Gustavo Pina Melgar wakiwa katika uso kwa uso

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad