CHUO CHA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (CATC) CHAPATA ITHIBATI YA KUTOA KOZI ZA USALAMA WA ANGA KIMATAIFA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 2, 2022

CHUO CHA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (CATC) CHAPATA ITHIBATI YA KUTOA KOZI ZA USALAMA WA ANGA KIMATAIFA

Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania  (CATC) kimekuwa miongoni mwa vyuo vilivyomo kwenye mtandao wa vyuo vya mafunzo ya usalama wa usafiri wa anga vipatavyo 35 duniani kote baada ya kufaulu tathimini iliyofanywa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO)  mapema mwezi July 2022.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa Cheti pamoja na Bendera ya ICAO Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari amesema mchakato wa tathimini ya chuo cha usafiri wa anga umeanza mwezi Aprili na kumalizika mwezi July 2022 ambapo chuo hicho kimefaulu vigezo vya kuwa chuo cha mafunzo ya Usalama wa Usafiri wa anga cha kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAF).

Amesema kuwa hatua hiyo inafanya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania kuwa miongoni mwa vyuo 6 vilivyoidhinishwa na kupata Ithibati ya ICAO kwaajili ya kutoa mafunzo ya usalama wa usafiri wa anga kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi (ESAF/ WACAF) ambapo vyuo vingine ni Dakar - Senegal, Douala - Cameroon, Johannesburg - Afrika ya Kusini, Lagos - Nigeria, Nairobi - Kenya.

"Mafanikio ya kuthibitishwa na kupata Ithibati hii kwa chuo chetu na kuwa miongoni mwa vyuo vya kikanda vya kutoa mafunzo ya usalama wa anga kunaenda sambamba na ongezeko la idadi ya wakufunzi watakaotoa mafunzo. Hadi sasa, Tanzania ina wakufunzi 21 waliothibitishwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (Certified National Aviation Security Instructors) Aidha, wapo wakufunzi wengine 9 ambao wamethibitishwa na ICAO (ICAO Aviation Security Certified Instructors) na wote ni Watanzania." alisema Johari

Pia amesema  kuwa hatua hii ya uthibitisho (Certification) inakifanya chuo hicho kuwa na hadhi ya kutoa mafunzo kimataifa kwenye eneo la usalama wa usafiri wa anga. Hii ni fursa ambayo italeta washiriki wa mafunzo hayo kutoka nchi mbali mbali duniani kulingana na mpango wa mafunzo wa chuo sambamba na mpango wa mafunzo utakaotolewa na shirika la usafiriwa anga Duniani yaani ICAO.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari(kulia) akikabidhiwa Bendera pamoja na muongozo wa Matumizi ya bendera ya Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) na Mwakilishi wa Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) upande wa Usalama wa Anga Afrika Justus Nyunja(kushoto) ambapo chuo hicho kimefaulu vigezo vya kuwa chuo cha mafunzo ya Usalama wa Usafiri wa anga cha kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAF) kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari(kulia) akikabidhiwa cheti cha kutambulika na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) na Mwakilishi wa Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) upande wa Usalama wa Anga Afrika Justus Nyunja(kushoto) ambapo chuo hicho kimefaulu vigezo vya kuwa chuo cha mafunzo ya Usalama wa Usafiri wa anga cha kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAF). 
Mwakilishi wa Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) upande wa Usalama wa Anga Afrika Justus Nyunja(kushoto) akionesha muongozo wa Matumizi ya bendera ya Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) itakayotumika kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) ambapo chuo hicho kimefaulu vigezo vya kuwa chuo cha mafunzo ya Usalama wa Usafiri wa anga cha kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAF) kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari akionesha Bendera pamoja na muongozo wa Matumizi ya bendera ya Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) mara baada ya kukabidhiwa kwa ajili ya kutumika kwenye Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) ambapo chuo hicho kimefaulu vigezo vya kuwa chuo cha mafunzo ya Usalama wa Usafiri wa anga cha kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAF) kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari akizungumza na wafanyakazi waTCAA, wafanyakazi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) pamoja na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhiwa Cheti pamoja na Bendela ya ICAO kwa ajili ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) ambapo chuo hicho kimefaulu vigezo vya kuwa chuo cha mafunzo ya Usalama wa Usafiri wa anga cha kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAF) kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam. 
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), wafanyakazi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari wakati wa hafla ya kukabidhiwa Cheti pamoja na Bendela ya ICAO kwa ajili ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) ambapo chuo hicho kimefaulu vigezo vya kuwa chuo cha mafunzo ya Usalama wa Usafiri wa anga cha kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAF) kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari, Mwakilishi wa Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO) upande wa Usalama wa Anga Afrika Justus Nyunja wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), wafanyakazi wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhiwa Cheti pamoja na Bendera ya ICAO kwa ajili ya Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) ambapo chuo hicho kimefaulu vigezo vya kuwa chuo cha mafunzo ya Usalama wa Usafiri wa anga cha kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAF) kwenye hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TCAA jijini Dar es Salaam.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad