HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 15, 2022

Bilioni tatu kujenga madaraja Mkuranga

 

Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewahakikishia wananchi wa Mkuranga kwamba serikali itajenga mwaka huu madaraja matatu yaliyoainishwa kwa ujenzi kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni tatu.

Waziri Ulega ameuambia mkutano wa hadhara hapa jana kwamba serikali imetenga fedha hiyo ili Jimbo la Mkuranga lifunguke kiuchumi. Bw Ulega ni mbunge wa Mkuranga.

Amewambia wananchi kwamba serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongwa na Rais Samia Hassan imetoa fedha hiyo kutekeleza ahadi yake ya kurahisisha usafiri na usafirishaji ili miradi ya maendeleo itekelezwe vizuri na kipato cha wananchi kiongezeke.

“Lengo la serikali ni kuliunganisha jimbo letu la Mkuranga na maeneo mengine ili kuinua uchumi wa jimbo letu. Tukiweza kufanya biashara kwa urahisi jimbo letu kufunguka kiuchumi,” alieleza Naibu Waziri Ulega na kufafanua kwamba Mkuranga itafunguka kiuchumi “kwa kuwa mazao tunayozalisha tutayafikisha sokoni kwa urahisi tofauti na hali ilivyo sasa kwani wananchi wanakabiliwa na adha ya usafiri na usafirishaji.”

Aliyataja madaraja yatakayojengwa kuwa ni daraja litakalounganisha Shungubweni na Marogolo na Kongo Mulanzi. Daraja la Msolwa litakalounganisha Kisahani naMalela na Nguja Kilamba mapaka Tipo. “Haya madaraji ni muhimku katika kulifungua jimbo letu kiuchumi,” alisema Bw.Ulega

Alialeza kuwa awali zilitengawa shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja likini kutokana na umuhumu wa miundombinu katika jimbo la Mkuranga Rais Hassan ameongeza fedha mpaka kufikia shilingi bilioni tatu kwa ajili ya maendeleo ya wilaya nzima ya Mkuranga. “Huu ni ushahidi wa dhamira ya serikali kumfikishia mwananchi maendeleo,” alisema.

Bw Ulega alitoa rai kwa wajenzi wa madaraja hayo kuyajenga kwa wakati, ufanisi na kutumia fedha kwa nidhamu ili ubora wa madaraja uendane na thamani ya fedha iliyotolewa. “Tujitahidi kutekeleza ujenzi kwa wakati na thamani ya fedha tuliyopewa ionekane. Tikiyatimiza haya itakuwa rahisi kupata fedha nyingine kutoka serikalini kwa ajili ya maendeleo ya jimbo letu,” alifanua.

Mkuranga inazalisha mazao ya kilimo ya bishara, mboga na matunda na bidhaa za uvuvi na misitu ambavyo vinatakiwa kufika sokoni kwa wakati ili kuongeza kipato cha wananchi na kuinua uchumi wa Wilaya ya Mkuranga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad