HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 29, 2022

ALIYEONA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMSABABISHIA KIFO MAMA YAKE

 

Njombe
Elina Nzilano bibi mwenye umri wa miaka 87 mkazi wa mtaa wa Idofi halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe anadaiwa kuuawa na mwanae Elisha Mwena (42) mwenye ulemavu wa macho (Kipofu) huku sababu ikitajwa kuwa ni bibi huyo kumnyima chakula mtoto wa mlemavu huyo (Mjukuu)

Ripoti ya awali ya jeshi la polisi inasema mlemavu huyo wa macho ambaye ni mtoto wa bibi Elina Nzilano alikasirishwa na kitendo cha mama yake kumnyima mwanae chakula huku sababu kubwa ya kutompa chakula ikitajwa kuwa ni kutokana na kitendo cha mjukuu wake kuiba kuku wake na kumla.

Kamanda wa polisi moka wa Njombe Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo “Mjukuu aliweza kuiba kuku na aliweza kumchinja na kumla peke yake na kummaliza, kitendo hiki kilimfanya bibi asimpe chakula sasa baba yake ambaye ni mlemavu akiwa amekaa pembeni wakati chakula kimeandaliwa hasira zilimkuta,alichukuwa fimbo yake na kuanza kumshambulia mama yake mzazi na kwa kuwa hawezi kujitetea alimjeruhi na kumpeleka hospitali ambako hakuweza kukaa hata siku mbili ingawa madaktari walijitahidi”amesema Kamanda Issah

Kamanda Issah amesema jeshi la polisi linamshikilia mlemavu huyo kwa ajili ya uchunguzi ili sheria ziweze kuchukuliwa na kufikishwa Mahakamani licha ya bwana Elisha kujitetea kutokupenda mtoto wake kuzuiwa kupata chakula.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad