HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 11, 2022

WAZIRI WA AFYA AHAMASISHA UCHANJAJI WA CHANJO YA UVIKO-19 MTWARA.

 

MTWARA - Tarehe 25 JULAI 2022 waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu na wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva akiwemo Harmonize, Marioo, Sholo Mwamba, Balaa Mcee, Sarafina, Mimi Mars, Mzee wa Bwax wameungana na umma wa Mtwara kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya chanjo ya UVIKO-19 katika uwanja wa Nyangwanda Sijaona.. Tukio hili limeandaliwa na Wizara ya Afya kupitia kitengo cha Elimu kwa Umma, pamoja na FHI 360 kupitia mradi wa EpiC kwa ufadhili wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

Malengo ya nchi ni kuchanja asilimia 70% ya wananchi wake kufikia mwishoni mwaka 2022, Mpaka kufikia tarehe 10 Julai Mtwara ilikuwa imechanja asilimia 29.3% ya wananchi wake . “Tunashukuru sana Serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassani kwa uamuzi wa kuwalinda wananchi wake dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO-19 na magonjwa mengine” alisema Ummy Mwalimu Waziri wa Afya. 


 

, Wizara ya Afya kupitia kitengo cha elimu ya Afya kwa umma kwa kushirikiana na wadau fhi360 unatumia tukio la kimuziki la Mziki Mnene likiambatana na kauli mbiu ya  Bega kwa Bega, Ujanja Kujanja” kuongeza kasi ya kutoa chanjo ya UVIKO-19.

“Kupitia Kampeni hii tunaendelea kukumbushana kukamilisha dozi, kusajliwa na kupata cheti cha chanjo ili kwa pamoja tufikie malengo ya kuikinga nchi yetu dhidi ya janga hili. Hivyo, ninawashukuru viongozi na wananchi wote mliofika hapa hii leo kushiriki uzinduzi huu pamoja na kuendelea kushirikiana kwa kuhamasishana sisi kwa sisi kutumia chanjo hizi. Vilevile, ninawashukuru FHI 360 na USAID Tanzania kwa kuandaa na kuwezesha shughuli hii.” Alisema Mheshimiwa Ummy Mwalimu.

Katika kuonyesha jinsi wadau wa maendeleo wanavyoshirikiana na serikali kuhakikisha inafikia malengo ya uchanjaji waliojiwekea na mikoa ambamo kampeni ya Mziki Mnene itatekelezwa, mwakilishi mkazi wa FHI 360 nchini Tanzania, Waziri Nyoni alisema; “chanjo ya UVIKO-19 imekuwa ni moja ya mkakati unaotekelezwa kwa msisitizo mkubwa zaidi baada ya kuzinduliwa rasmi nchini na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Julai, 2021. Kutokana na juhudi hizi zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau, kasi ya maambukizi ya UVIKO-19 imeendelea kupungua nchini. Kampeni ya kuhamasisha chanjo inatarajiwa kufanyika katika mikoa mitano ambayo ni Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe na Iringa.”

EpiC ni mradi wa kimataifa wa miaka mitano unaotekelezwa na shirika la FHI360 kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) pamoja na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), uliojikita katika kufikia na kuendeleza udhibiti wa janga la VVU/UKIMWI katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Hii ni kupitia kutoa msaada wa kitaalamu na huduma za moja kwa moja katika kuondoa vikwazo vilivyopo kufikia 95-95-95, na kuhamasisha usimamizi wa kujitegemea wa miradi ya VVU/UKIMWI kitaifa kwa kuboresha programu za utambuzi wa hali ya maambukizi ya VVU, kinga, matunzo na tiba.

#UjanjaKuchanja #TanzaniaInachanja

Hon. UMMY MWALIMU LAUCH A CAMPAIGN TO ENHANCE THE UPTAKE OF COVID-19 VACCINATION IN FIVE REGIONS.

Minister of Health and social welfare, honorable Ummy Mwalimu and number of Bongo Flava artists among them Harmonize, Marioo, Sholo Mwamba, Balaa Mcee, Sarafina, Mimi Mars, Mzee wa Bwax have join hand to raise awareness and sensitize on the COVID-19 vaccination uptake in Nyangwanda Sijaona stadium, Mtwara. This event-based COVID-19 vaccination campaign is prepared by the Ministry of Health through Health Promotion unit together with FHI 360, EpiC project with support from the United States Agency for International Development (USAID).

While Tanzania is required to vaccinate 70% of the population by the end of 2022, Mtwara is at 29.3% out of 70% of its population by 10th July 2022.

Event-based vaccination approach as an effective way to rapidly increase COVID-19 vaccination rates, EpiC is using music event “Mziki Mnene” with the theme “Bega kwa Bega, Ujanja Kujanja” to accelerate uptake of COVID-19 vaccine. Mziki Mnene platform will be used to provide education to Mtwara residents on COVID-19 vaccination, create demand and shot in the arm.

In her remarks honorable Ummy Mwalimu noted, “through Mziki Mnene platform we will continue to remind each other on completing the dose, to reach the goal of protecting our country against the pandemic. I would like to thank all the leaders and the citizen who are here to witness the launching of this vaccination campaign and for continuously cooperation in sensitizing on the vaccination uptake. I would also like to appreciate the FHI 360 and USAID Tanzania for making this possible.”

TThis campaign aims to ensure hard-to-reach people of Mtwara region who are more drived by Music to get shot into the arm. Also, opportunity to easily access vaccinations without the need to wait long in cue.

FHI360/EpiC is a five-year FHI 360 led global project funded by the U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) and the U.S. Agency for International Development (USAID) dedicated to achieving and maintaining HIV epidemic control, in the United Republic of Tanzania. This is through the provision of strategic technical assistance and direct service delivery to break through barriers to 95-95-95 and promote self-reliant management of national HIV programs by improving HIV case-finding, prevention, and treatment programming

#UjanjaKuchanja #TanzaniaInachanja

 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad