HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 20, 2022

WAVITA wafuata nyayo za Rais Samia Hassan Suluhu kwa vijana kujiajiri katika sekta ya kilimo

  Mwenyekiti wa WAVITA Shiganga George akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na vijana kujiajiri sekta ya kilimo katika majumuisho ya ya ziara ya nchi nzima kuhamasisha vijana kujikita katika sekta hiyo jijini Dar es Salaam.Makamu wa Mwenyekiti wa WAVITA, Irene Ngowi wa kwanza kutoka kulia Akizungumza namna vijana wa kike wanavyoweza kuingia katika sekta ya kilimo kutokana na kuwepo kwa masoko ya uhakika , jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
VIJANA Nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za Kilimo kwa kujiunga na Jukwaa la Wanasiasa Vijana Tanzania (WAVITA) na hiyo ikiwa ni kutokana na kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutoa mashamba kwa vijana na kuwapa hati ili kupitia kilimo waweze kuingia katika kujiajili wenyewe.

Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa WAVITA Shiganga George wakati akizungunza na waandishi wa Habari wakati wa kufanya hitimisho la ziara iliyofanyika Mikoa yote kwa miezi miwili.

Alisema kuwa ziara hiyo iliwalenga vijana wote nchini ambapo kila Mkoa walioenda waliwaeleaza vijana kujiunga na WAVITA ili waweze kuzungunza lugha moja, kuchangamkia fursa ya kilimo na kujiajili wenyewe kupitia msaada wa Rais pamoja na kuhakikisha wanatoa ushirikianao wakati wa zoezi la Sensa litakalofanyika Agosti 23, mwaka huu.

“Mama alisema amewapa mashamba vijana ili waingie katika kujiajiri kupitia kilimo na watapewa hati baada ya kukamilisha taratibu zote na sisi WAVITA tunawahamasisha vijana ili waingie kwenye uzalishaji kupitia kilimo hicho kwani Mama ameisha ona umuhimu wa vijana nchini na bila vijana nchi haiendi,”alisema Mwenyekiti na kuongeza

“Lakini katika kumsaidia Rais tumewaeleza vijana kwamba wanatakiwa kujituma kwani ikumbukwe kwamba hapa Nchini tuna vijana wa aina tatu, kuna wanaokaa vijiweni kwa ajili ya kukosoa pasipo kujali kazi inayofanyika, kunawalalamishi waliomaliza vyuo na aina ya tatu ni wale walalamishi hivyo WAVITA tunalenga kuwaleta pamoja ili tuzungumze lugha moja ambayo itakuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa Taifa letu kama vijana kuliko kuishia aina hizo tatu nilizozitaja.

Mwenyekiti Shiganga alisema, kuhusu suala la sense waliwaeleza vijana umuhimu wake na kwamba ni vyema sasa wakatoa ushirikiano wa hali na mali ili kufanikisha zoezi hilo ambapo kupitia hilo manufaa yatakuwa ni makubwa zaidi ikiwemo kuongezeka huduma za kijamii.

Makamu Mwenyekiti wa WAVITA Irene Ngowi alisema kuwa zoezi la kuwafikia vijana na kuzungunza nao masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo lilifanikiwa kutokana na kwamba kuna mabalozi nchi nzima.

“Tuna mabalozi nchi mzima hivyo tunaendelea kufanya uhamasishani ili vijana wasikae vijiweni badala yake wajitume ikiwa ni pamoja na kuchangamkia fursa ya kilimo ambayo iko wazi zaidi kutokana na msaada kutoka kwa Mama lakini pia kama vijana tunahakikisha tunamuunga mkono mama kwa kuzungunza lugha moja,” alisema Makamu Mwenyekiti.

Naye Muasisi na Mlezi wa WAVITA William Machum alisema kuwa tangu Rais Samia Suluhu Hassa aingie madalakani vijana wa vyama vyote wameungana na kuzungumza lugha moja na pia amewezesha kupatikana kwa fursa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kuongezeka kwa maendeleo Nchi nzima.

“Nadhani hilo sote tutakubaliana nalo lakini pia utafiti unaonesha kuanzia kidato cha nne , tano, sita hadi vyuo wote wanaomaliza wamekuwa wakitegemea kuajiliwa au anayesoma anategemea kuajiliwa hii haiwezekani kuajili watu wote hivyo cha kufanya WAVITA tunataka kuendela kuwashauli vijana tuungane ili tuzungumze lugha moja na tushauliane zaidi ikiwa ni pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na viongozi wakubwa akiwemo Rais,” alisema Mlezi Machum.

Alisema anachoshauri ni kwamba amebaini kuwa vijana wengi wako vijiweni na hawalipi kodi hivyo ni wakati muhafaka kwa vijana hao kuacha dhama hizo na kwenda kuwajibika.

Katibu Mkuu Gerevaz Kauzeni, alisema ni wakati muhafaka kwa vijana kuchangamkia fursa na kuacha kulalamika wala kusifia kwani wengine wamekuwa wakisifia vitu ambavyo siyo kweli na kwamba vingine vinakuwa havina sababu za msingi.

“Kwa mantiki hiyo sisi kama WAVITA tunataka kuhakikisha tunaungana kwa pamoja kuhakikisha tunamsaidia mama katika ujenzi wa Taifa lakini pia tupo kwa ajili ya kuwakomboa vijana kifikra ili waweze kufikia malengo,” alisema Katibu Kauzeni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad