KAMPUNI
ya Mbolea inayoongoza nchini ya Yara Tanzania, leo imekabidhi zawadi
kwa mshindi wa kampeni inayoendelea ya programu ya uaminifu iitwayo
YaraConnect. Katika tukio la leo muuzaji wa rejareja wa mjini Lushoto,
Bwana Hussein Kaniki, mmiliki wa duka la Kaniki Agrovet alizawadiwa
pikipiki mpya aina ya Boxer 150-UG yenye thamani ya shs milioni tatu.
Akizungumza
katika hafla ya utoaji zawadi, Meneja Masuluhisho ya Kidigitali wa Yara
Tanzania, Deodath Mtei alisema “Kaniki Agrovet alijikusanyia pointi
33,333 katika mauzo ya bidhaa za Yara na kisha kupiga picha stika
maalumu zinazowekwa juu ya mifuko wakati akiuza bidhaa kwa wakulima.
Muuzaji rejareja huyu akatumia pointi hizi kujishindia pikipiki yenye
thamani ya shs milioni tatu”.
Akaongeza
kwamba progamu hii huwapa pointi za uaminifu wauzaji wa rejareja
wanaponunua ama kuuza bidhaa za mbolea ya Yara ambazo zinaweza kutumika
kupata zawadi za pesa taslimu ama zawadi zisizo za fedha. “Kwa kuskani
msimbo (stika) maalumu (QR code) zilizowekwa juu ya mifuko wakati wa
kufanya mauzo ya bidhaa kwa wakulima, muuzaji wa rejareja anajikusanyia
pointi ambazo anaweza kuzitumia katika kujishindia pikipiki ama zawadi
nyingine ikiwa ni pamoja na kofia, fulana, chupa za chai, makoti, simu
za mkononi aina ya infinix, chupa za maji na pesa taslimu hadi kiasi cha
shs 3,600,000”.
Akawataka
wauzaji wa rejareja wote kuchangamkia fursa hii kupata taarifa zaidi
kuhusu bidhaa za Yara na pia kujishindia zawadi. “Kampuni imetenga
mamilioni ya shilingi kuwezesha programu hii na tutaendelea kuleta
masuluhisho mengine ya kidigitali ili kuhakikisha wadau wetu
wanafanikiwa,” alisema.
Kwa
upande wake Bwanashamba Mauzo wa Yara Kanda ya Kaskazini, Novatus
Salala alisema ndani ya programu ya YaraConnect kuna eneo lenye video za
maarifa na taarfia kuhusu matumizi bora na sahihi virutubisho vya
mazao. Muuzaji wa rejareja anaweza pia kupata taarifa zitakazoweza
kuwasaidia wakulima kutatua matatizo ya ukosefu wa virutubisho
unaoathiri uzalishaji lakini pia kuweza kusimamia akiba zao vizuri.
Akizungumza
muda mfupi mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake, Bwana Kaniki alisema
anayo furaha kubwa na kuishukuru Yara kwa msaada wao na kwa kuwakumbuka
wauzaji wa rejareja. “zawadi hii imenipa hamasa kubwa, naishukuru Yara
kwa kuendelea kujitolea kuwasadia wauzaji wa rejareja. Nitaendelea kuuza
bidhaa za Yara kwa bidii nyingi na natoa wito kwa wauzaji wengine
kujiunga na YaraConnect”, alisema Bwana Kaniki.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Yara, Bwana Winstone Odhiambo naye alisema kampuni
itaendelea kuhakikisha kunakuwa na mbolea bora, ya kutosha na yenye bei
nafuu katika soko. Akiukaribisha mpango wa mbolea ya ruzuku ya serikali
akisema utasaidia sana katika kuhakikisha wakulima wanapata ahueni
kutoka katika makali ya sasa ya bei.
Bwana
Odhiambo anasema; Wauzaji wa rejareja wa Yara wana kila sababu ya kuwa
na uhakika wa msaada na ushirikiano wetu endelevu katika kuhakikisha
bidhaa zetu zote zinapatikana kwa wakati katika soko. Programu ya
YaraConnect ni moja ya juhudi za kampuni katika kuwatambua na kurudisha
shukurani kwa wateja wetu wa thamani.”
Programu
yara Connect ilizinduliwa Julai 1, 2021 ikiwa na lengo la kutoa msaada
wa kiufundi kuhusu masuala ya kilimo na matumizi bora ya mbolea za Yara,
kuwapa wauzaji wa rejareja kujifunza na kupata majibu ya maswali kuhusu
kilimo na matumizi sahihi ya bidhaa za Yara na pia kupata msaada kwa
mteja kupitia program hiyo.
Programu
inapatikana kote kupitia play store kwa watumiaji wa simu za android
ama apple store kwa watumiaji wa IOS. Kwa taarifa zaidi wauzaji wa
rejareja wanaweza kutembelea mitandao ya kijamii (yaratanzania), ama kwa
tovuti www.yara.co.tz au kwa kupiga simu bila malipo katika kituo cha huduma kwa wateja kwa namba 0800750188.Meneja
Masuluhisho ya Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania,
Deodath Mtei (kulia), akikabidhi zawadi ya pikipiki mpya aina ya Boxer
150-UG yenye thamani ya shs milioni 3 kwa mshindi wa kampeni ya Programu
ya uaminifu ya YaraConnect, Hussein Kaniki (wa tatu kushoto), mmiliki
wa duka la Kaniki Agrovet, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika
dukani kwake katika Kijiji cha Manolo, Tarafa ya Mlalo, Wilaya ya
Lushoto, mkoani Tanga jana.
Bwanashamba
Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania,
Novatus Salala (kushoto), Bwanashamba mwingine wa Yara, Omary Hussein
(katikati), na mshindi wa kampeni ya uaminifu ya yaraConnect, Hussein
Kaniki (wa pili kushoto), wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa ghala la
kuhifadhia mbolea la duka la mshindi huyo katika hafla ambayo Yara
ilimkabidhi Bwana Kaniki pikipiki yenye thamani ya shs milioni 3 ikiwa
ni zawadi ya ushindi wa kampeni ya YaraConnect inayoendelea. Kulia ni
Meneja Masuluhisho ya Kidigitali, Deodath Mtei na Mratibu wa Miradi ya
Kidigitali, Eliwaza Mzonge.
Meneja
Masuluhisho ya Kidigitali wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania,
Deodath Mtei (kulia), akizungumza katika hafla ambayo Yara ilimkabidhi
Bwana Hussein Kaniki (wa pili kushoto), mmiliki wa duka la Kaniki
Agrovet, pikipiki yenye thamani ya shs milioni 3 ikiwa ni zawadi ya
kampeni ya uaminifu ya yaraConnect katika hafla iliyofanyika katika
Kijiji cha Manolo, Tarafa ya Mlalo, Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga
jana. Wengine ni wafanyakazi wa Yara.
Bwanashamba
wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Omary Hussein (kulia),
akizungumza katika hafla ambayo Yara ilimkabidhi Bwana Hussein Kaniki,
mmiliki wa duka la Kaniki Agrovet, pikipiki yenye thamani ya shs milioni
3 ikiwa ni zawadi ya kampeni ya uaminifu ya yaraConnect katika hafla
iliyofanyika katika Kijiji cha Manolo, Tarafa ya Mlalo, Wilaya ya
Lushoto, mkoani Tanga jana.mshindi
wa kampeni ya uaminifu ya yaraConnect, Bwana Hussein Kaniki, mmiliki wa
duka la Kaniki Agrovet, akitoa shukurani zake kwa Kampuni ya Mbolea ya
Yara Tanzania, mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki mpya yenye
thamani ya shs milioni 3 baada ya kuibuka mshindi wa kampeni hiyo
inayoendelea. Aliwata wauzaji wenzake kujisajili na programu ya
yaraConnect ili waweze kushinda zawadi kama yeye.
Baadhi
ya wakazi wa Kijiji cha Manolo, Tarafa ya Mlalo, Lushoto, mkoani Tanga,
wakimsikiliza Bwanashamba Mauzo wa Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya
Mbolea ya Yara Tanzania, Novatus Salala (katikati), akizungumza kuhusu
faida na matumizi sahihi ya Mbolea bora ya Yara, katika hafla ya
kukabidhi zawadi ya pikipiki yenye thamani ya shs milioni 3, kwa mshindi
wa kampeni ya uaminifu ya yaraConnect, Bwana Hussein Kaniki wa dula la
Kaniki Agrovet lililopo kijijini hapo. Makabidhiano yalifanyika kijijini
Manolo Jana.
No comments:
Post a Comment