HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 16, 2022

UTAJIRI WASABABISHA AHUKUMIWE KWENDA JELA MIAKA 30

 

Njombe
MAHAKAMA ya wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe imemhukumu kutumikia kifungo cha mika 30 jela Joseph Mwajombe (33) mkazi wa kijiji cha Lulanzi kwa kosa la kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 15.

Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahaka ya wilaya hiyo James Mhoni ameeleza kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 7, mwaka huu ambapo alikuwa anakwenda shuleni na pikipiki kumfuata binti yake huyo lakini akakutana nae njiani ndipo akampakia kwenye pikipiki na mpaka eneo la jirani na nyumbani kwao.

Amesema katika eneo hilo kuna bwawa ambalo liko jirani ndipo akachepuka naye katika eneo la bwawa hilo na kumuambia binti yake kuwa amewasiliana na freemason ambao walibandika tangazo lao kwenye nguzo ya umeme hivyo wamemwambia afanye mapenzi na binti yake ndipo atapata utajiri hivyo alimuomba binti yake huyo akubali kufanya nae mapenzi.

Ameongeza kuwa binti yake huyo alikataa kufanya hivyo ndipo mtuhumiwa huyo alimpiga na kumuingilia kimwili kwa nguvu na baada ya kutiza lengo lake alimrudisha binti yake huyo nyumbani kisha akaondoka kuelekea kusiko julikana.

Hakimu Mhoni amesema ilipofika majira ya usiku binti huyo alianza kulia huku akimwambia mama yake kuwa haitaji kuendelea na shule na alipoulizwa sababu alieliza alichofanyiwa na baba yake ndipo mama yake huyo akachukua hatua ya kutoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji ambapo mtendaji alichukua mgambo na kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituoni ambako alikiri kutenda kosa hilo.

Awali mwendesha Mashtaka Abraham Kamwela aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wote wenye tabia kama hizo .

Hakimu Mhoni amesema amesikiliza ushahidi wa pande zote mbili na huku ushahidi wa upande wa mashtaka ukionekana kuwa na nguvu na kuamua kutoa hukumu hiyo kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 130 (1) (2) (e) na 131 (1) cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya 2019.

Aidha katika utetezi wake mtuhumuwa huyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwakuwa ana watoto 3 wenye umri chini ya miaka 18 wanaomtegemea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad