TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE NA UNA TANZANIA ZAANDAA MAFUNZO KUADHIMISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI 2022 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 30, 2022

TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE NA UNA TANZANIA ZAANDAA MAFUNZO KUADHIMISHA SIKU YA VIJANA DUNIANI 2022


 

DAR ES SALAAM AGOSTI 30, 2022: Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) ikishirikiana na Asasi ya Umoja wa Mataifa (UNA) Tanzania na wadau mbalimbali itakutanisha Jumla ya vijana 150 katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuimarisha biashara na kazi endelevu za mashirika ya Vijana mnamo tarehe 2 na 3 Septemba, 2022 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es salaam.

Mafunzo hayo, ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Vijana duniani (IYD2022), yatakuwa jukwaa la kufichua fursa na rasilimali kwa vijana ambazo zitasababisha kukuza upatikanaji wa kazi zenye staha na kukuza ushiriki wao bora kwenye masuala yanayowahusu. Kitaifa maadhimisho haya yalifanyika tarehe 12 Agosti, 2022 kaulimbiu ikiwa “Kila Mmoja Anahusika Kujenga Uchumi Imara, Ustawi Na Maendeleo Endelevu: Jiandae Kuhesabiwa”

“Kutakuwa na mafunzo ya kusisimua kutoka kwa wataalam waliobobea katika sekta binafsi na asasi za kiraia. Mafunzo haya ambayo yameandaliwa kwa pamoja na vijana, yatatumika kuchochea ujuzi na maarifa, ushauri kutoka kwa wabobezi katika sekta husika ili kuongoza mazungumzo baina ya vizazi. Maeneo ya mafunzo yaliyoainishwa katika programu yalipendekezwa na zaidi ya vijana 50 kutoka sekta binafsi na za kiraia”,anamasema Mtendaji Mkuu wa JMKF Bi. Vanessa Anyoti.

Bi. Anyoti anaongezea kwamba: “Siku ya Vijana Duniani imekua jukwaa muhimu la kuthamini mchango mkubwa wa vijana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Tanzania inaungana na mataifa mengine Wanachama wa Umoja wa Mataifa kujadili, kusherehekea na kutambua nafasi ya Vijana katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, kutoa mapendekezo na kuonesha uwezo wa vijana.

Hii, inatokana na ukweli kwamba, vijana ndio kundi kubwa katika jamii yoyote ile. Vijana ndio wenye nguvu zaidi ya kufanya kazi, Vijana ni wabunifu, Vijana ndio chachu ya mabadiliko chanya katika jamii na Vijana ndio walinzi wa historia na warithi wa Mataifa yao”, anafafanua.

Kwa taarifa Zaidi wasiliana na Nicholaus Luoga kupitia 0759506122 na kupitia nicholaus.luoga@jmkfoundation.org


MAELEZO YA MAADHIMISHO KWA UFUPI

Jina la Tukio

Maadhimisho ya Siku Ya Vijana Duniani 2022

Tarehe

Muda

2-3 Septemba 2022

Saa 3.00 Asubuhi

Mahali

Makumbusho ya Taif ana Nyumba ya Utamaduni, Dar es Salaam

Waandaaji

Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete wakishirikiana na UNA Tanzania.

Wawasilishaji Mada

UWEZESHAJI, UNA Tanzania,  institute of Directors Tanzania (IoDT), Foundation for Civil society (FCS), LSF, Prudence Zoe Glorious Impact firm, PACT.

Nani anaweza kushiriki?

Vijana 150 wanaomiliki biashara na waliokua na asasi za kiraia.

Lugha itakayotumika

Lugha ya Kiswahili, japo baadhi ya mada zitachanganya lugha kulingana na aina ya wawasilishaji mada watakaokuwepo.

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad