Pichani kushoto ni Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh Rosemary Senyamule pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Tanzania, David Minja kwa pamoja wakizindua muonekano mpya wa sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi kwenye hafla fupi iliofanyika leo jijini Dodoma.
MKUU
wa Mkoa wa Dodoma My Rosemary Senyamule ameipongeza Kampuni ya Unilever
ambayo ni watengenezaji wa Sabuni ya Omo kwa namna ambavyo wamekua
mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali katika mambo ya kijamii.
Mh.
Senyamule ametoa pongezi hizo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa
muonekano mpya wa Sabuni ya Omo iliyoboreshwa zaidi ambapo amesema
Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wawekezaji wanaokuja kuwekeza
nchini.
Mh. Senyamule amesema Kampuni ya Unilever kupitia bidhaa
yake ya Omo wamekua wadau wakubwa wa Serikali na Watanzania kwa ujumla
na kwamba anafarijika kuona wakizindua muonekano mpya wa Sabuni hiyo.
"
Wote tunatambua ya kwamba Unilever ni kampuni kubwa na ya kimataifa
ambayo bidhaa zake wengi wetu humu hutumia kila siku. Kuna sabuni ambazo
kila siku tunatumia kwenye kufua, mafuta ambayo kila siku tunajipaka na
royco ambayo ukitaka mboga iwe tamu lazima tutumie.
Bidhaa za
Unilever ni bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na zimekidhi vigezo vyote
vya kimataifa. Ninayo furaha kushiriki kwenye uzinduzi huu wa muonekano
mpya wa sabuni ya Omo iliyoboreshwa zaidi," Amesema Mh Senyamule
Amesema
Unilever Tanzania na Sabuni yao ya Omo wamekuwa Mstari wa Mbele katika
kushiriki mambo ya Kijamii katika mkoa wetu wa Dar es salaam hususani
katika kutoa Msaada wa Shuka Pamoja na sabuni kwenye Hospital za
Muhimbili Hospitali, Mwananyamala Hospitali na Amana Hospitali zilizopo
jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Unilever Tanzania, David Ninja amemshukuru Katibu Tawala Uchumi na
Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam,Mkuu wa mkoa wa Dodoma na serikali
kiujumla kwa kufika kushiriki tukio hilo la uzinduzi wa muonekano mpya
wa Sabuni ya Omo ambapo pia amewahakikishia watanzania kwamba ubora wa
bidhaa hiyo umeongezeka maradufu.
" Kampuni ya Unilever imekuwa
ikienda sambamba na ukuaji wa teknolojia duniani ili kuendana na hali ya
soko na hususani kwa wateja wake.
hivyo leo ni siku muhimu
sana kwetu kwani tunazindua muonekano mpya wa sabuni ya Omo
iliyoboreshwa zaidi kwa lengo la kuendelea kuvutia watumiaji wa sabuni
hii.
Naomba nichukue fursa hii kuwaambia wateja wetu na jamii ya
Kitanzania kwamba ujumbe wetu kwa leo ni kuwa OMO NI MKALI WA MADOA SUGU
ni sabuni namba moja kwa kuondoa madoa sugu na kwa haraka zaidi kwani
unga na vimeng’enya viliyomo ndani mwake ni mzuri na huondoa uchafu kwa
haraka Zaidi na kuacha nguo yako ikiwa na harufu nzuri (manukato) ndani
ya siku 14," Amesema Minja.
Amesema Kampuni ya Unilever kwa
kupitia sabuni yake ya Omo imekuwa mstari wa mbele katika kurudisha kile
kidogo tupatacho kwa watanzania na kuungana na watanzania katika
kujenga Maisha bora kwa wote.
" Tumekuwa na kampeni mbalimbali
kama MKONO WA SHUKRANI, kwa mwaka jana, kampeni hii ilifanyika katika
Hospitali tatu jijini Dar es salaam Muhimbili, Mwananyamala Pamoja na
Hospitali ya Amana, ambapo tulichangia mashuka Pamoja na sabuni kwa
ajili ya watanzania wenzetu, Pia Omo tumekuwa na kampeni ya Mkono Wa
Ukarimu, kampeni maalum kabisa wakati wa kipindi cha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani kampeni hii ilifanyika na tulikusanya nguo kutoka kwa
watanzania wenzetu na tukafua kwa kutumia Omo na pia tukaenda
kuzikabidhi kwa wale watu wenye uhitaji," Amesema.
No comments:
Post a Comment