BENKI ya CRDB yadhamini michuano ya Gofu ya "Corporate Masters" - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 9, 2022

BENKI ya CRDB yadhamini michuano ya Gofu ya "Corporate Masters"

  
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya CRDB, Stephen Adili (kulia), akimkabidhi zawadi ya kombe na vifaa vya mchezo wa Gofu mshindi wa jumla wa mashindano ya "Corporate Masters", Hussein Dewji, wakati wa fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.  Benki ya CRDB ilikuwa ni miongoni mwa wadhamini wa mashindano hayo. Kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Maalum, Gibson Mlaseko.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro akitupa mpira shimoni wakati wa mashindano ya mchezo wa gofu ya "Corporate Masters" ikiwa ni hatua ya fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mashindano hayo yalifanyika kwa udhamini wa makampuni mbalimbali yaliongozwa na Benki ya CRDB.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michzo, Nape Nnauye (kulia) akibadilishana mawazo na mdau wa Mchezo wa Gofu (jina kapuni) wakati wakiwa kwenye mashindano ya "Corporate Masters" ikiwa ni hatua ya fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Katiba na Sheria Damas Ndumbaro (wa tatu kushoto), Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michzo, Nape Nnauye (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa fainali ya mashindano ya Gofu ya Corporate Masters yaliyodhaminiwa na Benki ya CRDB.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad