VETA yagundua dawa za asili kuua magugu na wadudu wahalibifu Shambani - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 3, 2022

VETA yagundua dawa za asili kuua magugu na wadudu wahalibifu Shambani


*Wakulima watazalisha kwa tija na kukua kiuchumi

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
MAMLAKA ya Elimu n a Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kupitia Chuo cha VETA Chang'ombe wamegua Dawa za asili ya kupulizia na kuua magugu na wadudu mashambani.

Wakulima wamekuwa na changamoto katika kilimo na wakati mwingine kuwa na ukosefu wa fedha na kusababisha mazao kuharibika mashambani sasa dawa za asili za kuua magugu zinapatikana na zimebuniwa na wazawa kutoka VETA .

Amesema kuwa kazi yao ni kufanyia utafiti changamoto za jamii mwaka jana waliweza kuja na suluhu ya kuua bakteria katika vyoo ambao wanaosababisha ugongwa wa maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) ambapo jamii wanatumia

Akizungumza katika maonesho ya 46 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba) Mwalimu wa Chuo cha VETA Chang'ombe Ally Issa amesema kuwa waliamua kufanya utafiti na kubaini hakuna dawa ya kuua magugu mashambani ambazo si za asili ambapo wametafiti na kutengeneza kila mtu anaweza kumudu gharama.

Amesema wamegundua dawa mbalimbali ambazo zimeweza kusaidia jamii na hakuna madhara yanayopatikana kwa kutumia dawa hizo.

Issa amesema kuwa dawa hiyo iko katika uangalizi na Mmalaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) katika hatua mwisho wakiwa wamepata cheti cha uchunguzi na kibali cha muda cha Maonesho ikiwa tayari itaingia sokoni.

Aidha amesema kuwa VETA inaangalia nguvu kazi ambapo watu wakiwa na changamoto za kiafya hawawezi kuzalisha na hatimae Taifa haliwezi kupata mapato kutokana na nguvu kazi hiyo.

VETA Chang'ombe licha ya kufundisha katika Mafunzo mbalimbali wanaangalia changamoto zinazowakabili jamii na kutafuta suluhisho.

Amesema kutokana na Kauli mbiu ya maonesho 45 ni Uchumi wa Viwanda kwa ajira na biashara endelevu inasaidia vijana kupata ajira kwa kupata Mafunzo ya utengenezaji wa dawa hiyo na kuingiza sokoni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad