HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 8, 2022

SERIKALI, WADAU KUSHIRIKIANA KUWEKA MATUMIZI SAHIHI YA MATUMIZI YA MAJI

 

IMEELEZWA kuwa changamoto ya maji kwa matumizi ya kilimo,mifugo na viwanda itaendelea iwapo serikali na wadau wa sekta ya maji hawatochukua hatua stahiki za kuweka mazingira rafiki ya matumizi sahii ya rasilimali hiyo ambayo imetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa kupitia sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, mifugo, viwanda na Biaashara.

Hayo yameelezwa kwenye jukwaa la uhakika wa maji lililofanyika Jijini Dodoma lililokuwa na ajenda kuu ya ufadhili wa rasilimali fedha kwa usalama wa maji ili kuboresha maisha ya wakulima wadogo na ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Jukwaa hilo liliandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la shahidi wa maji kupitia mradi wake wa utafiti wa UHAKIKA WA MAJI((Fair Water Future ) unatekelezwa kwenye Wilaya mbili za Kilosa na Kilombero mkoani Morogoro, wenye lengo la kutambua uwajibikaji wa viongozi wa serikali katika kutatua changamoto za upatikanaji wa maji kwa shughuli za kilimo,mifigo na uvuvi.

Akizungumza kwenye jukwaa hilo Mwenyekiti wa Taifa wa bodi ya maji Mhandisi Mbogo Futakamba alisema Bado kuna uelewa mdogo kwa wananchi juu ya mchango wa maji kwenye uchumi wa taifa hivyo kuna haja ya serikali kwa kusirikiana na wadau wa maji kutoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi sahihi ya maji kwenye uchumi kwani kila sekta inategemea uwepo wa maji ili iweze kuzarisha na kuchangia pato la nchi.




“Maji yana

kupa usalama wa elimu, afya, chakula na nishati kikubwa zaidi maji yanakupa usalama wote, tuna msemo wetu ambao unasema usalama wa maji ni usalama wa Tiafa. Tusipo yaelewa hayo tutajua maji ni kudra aliyotupa mwenyezi mungu tukayatumia kadri yanavyohitajika bila ya kujua maji yanakwisha.”Alisema Mhandisi Futakamba.

Aliongeza Bodi ya maji inakazi ya kuwakutanisha wadau wote wa maji ili kujadili kwa pamoja namna bora ya kuweka usawa wa watumia maji bila ya kuathili mazingira.

Aidha amewataka wananchi kutumia fursa zitokanzo na mabadiliko ya tabia nchi hasa katika kipindi cha mvua nyingi kwa kuhifadhi maji ili yaweze kuwasaidia kwenye kipindi cha ukame kwenye shughuli mbalimbali kama kilimo na ufugaji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mashahidi wa maji Mhandisi Herbert Kashililah alisema lengo la jukwaa hilo ni kubadilishana uzoefu na kutoa uelewa kwa wadau wa maji kuhusu usimamizi wa rasilimali hiyo pamoja na kuweka mkakati wa namna gani wanaweza kufanya uwekeaji katika sekta ya maji kwa kutumia mifumo na fursa zilizopo.

Alisema kupitia tafiti walizozifanya kwenye Wilaya ya Kilosa na Kilombero mkoani Morogoro wamebaini kuna mfumo unaozibana taasisi, mabonde ya maji na mamlaka zilizopewa dhamana kushindwa kutekeleza na kusimamia sera na sheria zilizopo



Kutokana na changamoto hiyo Mhandisi Kashililah ameiomba serikali kufanya marekebisho ya mfumo uliopo ili kutoa fursa kwa Taasisi na mamlaka kufanya kazi kwa uhuru hali itakayosaidia kuweka usalama wa maji na utuzaji wa mazingira.

Tafiti zao pia zilionesha uchafuzi na uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya maji ambao utapelekea upungufu wa upatikanaji wa maji endelevu kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi.

Mkurugenzi wa uratibu wa program na usimamizi wa mazingira kutoka Wizara ya maji Mhandisi Dorisia Mulashani alisema jukwaa hilo litatoa fursa kwa wizara ya maji kujua namna gani wanaweza kushirikiana na wadau katika kupata rasilimali fedha zitakazosaidia kutunza vyonzo vya maji na kuwa na uhakika wa maji kwa taifa.

Akizungumzia mradi wa uhakika wa maji Mkurugenzi wa shahidi wa maji Bwana Abel Dagange alisema mradi huo unalenga kutoa elimu kwa wananchi ya namna wanavyoweza kujisimamia na kuwasilisha changamoto zao kwa viongozi wa serikali kwa njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na kuandika barua kwa viongozi hao.

Alisema kupitia mradi huo baadhi ya wakulima, wavuvi na wafugaji wa wilaya za Kilombero na Kilosa waliofikiwa moja kwa moja na mardi kupitia mshahidi wa maji wamenufaika kwa kupata elimu aliyowasaidia kutatua changamoto zao zilizokuwa zinawakabili.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad