Sehemu
ya washiriki wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa maarufu
Sabasaba wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutembelea Hifadhi ya
msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi uliopo wilayani Kisarawe
mkoani Pwani.
Na Mwandishi Wetu
WAKALA
wa Huduma za Misitu Tanzania umesema tangu ilipozinduliwa filamu ya
Royal Tour na Rais Samia Samia Suluhu Hassan idadi ya watalii
wanaotembelea utalii Ikolojia imeongezeka kutoka watalii 49,000 kwa
mwaka hadi kufikia 150,000.
Umesema kutokana na kuongezeka kwa
Wakala huo nao umeamua kuweka mikakati ya kuendelea kuboresha
miundombinu ya hifadhi hizo ikiwemo kuboresha njia za kupita
watalii,maeneo la malazi pamoja na kuwepo kwa maeneo mazuri ya
kupumzikia.
Hayo yameelezwa leo Julai na Mkuu wa Kitengo cha
Uhamasishaji Utalii katika Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
Anna Lauwo wakati washiriki wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa
walipotembelea Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi
ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia kutangaza sekta
ya utalii kupitia filamu ya Royal Tour pamoja na kuhamasisha utalii wa
ndani.
"Filamu ya Royal Tour imeongeza watalii kwa kiasi kikubwa
na TFS imeongeza watalii wengi wa ndani pamoja na nje ,kwa mfano mwaka
jana kabla ya Royal Tour idadi ya watalii ilikuwa inaanza 49000 lakini
baada ya hii Royal Tour tumepata watalii 150,000.
"Ongezeko ni
kubwa sana na katika kipindi kifupi, kwa hiyo unaona hii Royal Tour
imehamasisha wengi kufahamu kumbe kuna utalii, kumbe Tanzania kuna kitu
cha pekee ambacho sehemu nyingine hakipo na watu wameamka kumbe kuna
umuhimu wa kwenda kupumzika , " Lauwo.
Kutokana na ongezeko hilo
Lauwo amesema TFS wamejipanga vizuri kabisa akitoa mfano katika misitu
yao yote nchini ukiwemo Pugu wameboresha miundombinu kama njia za
kuingilia msituni ,wameboresha ya maegesho ya magari, wameboresha malazi
kwa kujenga maeneo ya malazi na kuboresha yale yaliyopo kwa ajili ya
kukidhi mahitaji.Aidha wanahamasisha wawekezaji wa ndani na nje kuja
kuwekeza kwenye huduma za malazi na chakula hasa loji ambazo haziharibu
mazingira na makambi.
Kuhusu Msitu wa Pugu amesema msitu huo uko
wilayani Kisarawe Kanda ya Mashariki na ni msitu ni moja kati ya Misitu
23 inayosimamiwa na TFS ambayo imepandishwa hadhi kutoka Misitu ya
asili na kuwa msitu wa Mazingira asilia kutokana na uwepo wa viumbe na
mimea adimu ndani ya Misitu hiyo ambavyo havupatikani maeneo mengine
ulimwenguni.
Amefafanua katika misitu hiyo 23 kuna vivutio vya
aina mbalimbali ikiwemo maporomoko ya maji ambayo ni ya pili kwa urefu
katika Bara la Afrika yenye urefu wa mita 235 yanayopatikana hifadhi ya
Kalambo.
Pia amesema kuna utalii mwingine unaofanyika kwenye
mashamba ya miti yanayosamiwa na TFS akitokea mfano utalii wa kuendesha
baiskeli, mazuri kwa mbio za farasi na kutembea kwa miguu msituni.
"Kwa
hiyo kwenye mashamba hayo Kuna maporomoko kwa mfano Meru Usa kuna
maporokoko ya maji yenye urefu wa mita 70 lakini hayo watu hawayajui
wakati yapo karibu kabisa na Mji wa Arusha ,ni sehemu nzuri ambayo watu
wanaweza kwenda kutembea na kurudi.
"Katika hii misitu yetu
tunayofanya utalii Ikilojia haturuhusu kufanya shughuli nyingine yoyote
isipokuwa utalii Ikilojia,utafiti pamoja na mafunzo na ndani ya hii
Misitu tunahimiza sana uhifadhi wa mazingira kwasababu ndio kivutio
kikubwa na hakuna kuangusha aina yoyote ya takataka wala kuchukua mdudu
au mmea wa aina yoyote.
Akielezea zaidi amesema utalii Ikilojia
ni zao jipya la utalii nchini ambalo halijulikani na wengi lakini
linamanufaa makubwa katika ya binadamu kwasababu ni maeneo tulivu na
yenye hewa safi na ndio sehemu pekee unayoweza kupumzika na kuondoa
msongo wa mawazo.
Pamoja na hayo Lauwo wamewahimiza Watanzania
watembelee msitu wa Hifadhi ya mazingira Pugu Kazimzumbwi ambao uko
karibu kabisa na Dar es Salaam, unaweza kwenda na kurudi lakini ukitaka
kulala yako maeneo ya malazi.
Akielezea faida za Msitu wa Pugu
mbali ya utalii amesema kuna hewa safi kabisa ambayo Dar es Salaam
huwezi kuipata."Msitu huu tunasema ni mapafu ya Dar es Salaam,na
tunafahamu kwa sasa hivi tunasema hali ya hewa imebadlika sana
"Na
saa zingine hewa inakuwa joto au baridi sana.Hayo yote ni mabadiliko ya
tabianchi lakini kuifanya hewa irudi kama awali tunahimiza uhifadhi wa
misitu.Kwasababu Msitu wenyewe kama ulivyo unavuta hewa chafu na kutoa
hewa safi ndio maana tunaita mapafu ya Dar es Salaam."
Kuhusu
viingilio amesema mtu mzima ni Sh.2000 lakini wenye umri wa miaka Sita
hadi miaka 17 ni Sh.1000 na walio na umri kuanzia miaka mitano kushuka
chini ni bure.

No comments:
Post a Comment