HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 22, 2022

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN PAMOJA NA RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA WAFUNGUA BARABARA YA KIKANDA YA AFRIKA MASHARIKI (ARUSHA BYPASS KM 42.4) JIJINI ARUSHA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imepanga kuimarisha sekta ya bandari na sekta ya anga ili kukuza biashara ndani ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.


Rais Samia amesema hayo leo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass) yenye urefu wa kilomita 42.4. ambayo imegharimu shilingi Bilioni 197. 4.


Aidha, Rais Samia amesema barabara hii ni muhimu kwa nchi yetu kwa kuwa ni sehemu ya barabara kuu inayounganisha kanda ya Kaskazini (Northern Corridor) hadi Holili Taveta mpakani mwa Tanzania na Kenya kuelekea Voi nchini Kenya. 


Barabara hii pia inaunganisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga na Kanda mbalimbali zinazounganisha Tanzania na nchi jirani za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Zambia Sudani Kusini na Sudani hadi Ethiopia.


Vile vile Rais Samia amesema kukamilika kwa barabara hii kumeimarisha sekta ya utalii pamoja na ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii katika mikoa inayopita, nchi kwa ujumla, pamoja na nchi jirani. 


Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) katika Sherehe zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) uliofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wakati wa Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.

Kwaya ya Utumishi ikitoa burudani katika Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.


Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) zilizofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha tarehe 22 Julai, 2022.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad