Benki ya NMB katika
kuhakikisha Sekta ya utalii visiwani Zanzibar inaimarika, imekabidhi
Mashine za malipo (POS) 50 pamoja na Lipa Mkononi (QR) kusaidia
kudhibiti na kukuza ukusanyaji mapato katika Sekta ya Utalii visiwani
Zanzibar.
Akizungumza katika hafla ya
makabidhino, Mkuu wa Idara ya Biashara za Kadi NMB - Philbert Casmir
alisema “huu ni utekelezaji wa makubaliano tuliofanya miezi sita
iliyopita kati ya Benki ya NMB pamoja na Wizara ya Utalii na Mambo ya
Kale Zanzibar - Tulisaini makubaliano ya kuimarisha uchumi wa bluu kwa
kutoa elimu na kuhamasisha watu kutembelea vivutio vya kitalii".
Akipokea
mashine hizo pomoja na Lipa Mkononi (QR) Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Dk. Amina Ameir Issa alisema kuwa
Benki ya NMB imerahisisha malipo, sasa unamiza malipo kidijitali kwani
ukienda kwenye vituo vya utalii huna haja ya kubeba fedha taslimu. Uwe
Mtanzania au mgeni, unalipia kwa mashine hizi kwa kutumia kadi yako ya
benki, ambayo ina pokea mifumo ya MasterCard, VISA na UnionPay au simu
za mkononi kutumia mfumo wa Ku-scan au Lipa Namba kufanya malipo.
Aidha,
alieleza kuwa sasa Serikali itaweza kujua kiwango cha fedha
kinachoingia kwa siku, wiki, mwezi au mwaka hivyo kuwawezesha kufikia
malengo ya mwaka huu wa fedha ya kukusanya Sh. Bilioni Moja katika sekta
ya utalii. Maeneo yatakayotumia mfumo huu ni pamoja na Mvuleni,
Kizimkazi, Mapango ya watumwa Manga Pwani, Bi Khole, Mtoni, Rasi ya
Kibweni na Maruhubi.
Mkuu
wa Biashara ya Kadi Benki ya NMB - Philbert Casmir (katikati),
akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar
- Dk. Amina Ameir Issa, mfano wa mashine ya kupokea malipo kwa ajili
ya wizara hiyo, NMB imekabidhi mashine 50 ambazo zitasaidia kuimarisha
na kukuza ukusanyaji wa mapato kwenye Sekta ya Utalii. Kutoka kushoto ni
Meneja Mwandamizi Biashara ya Kadi NMB - David Ngusa na Meneja Biashara
NMB Zanzibar - Naima Said Shame..
Mkuu wa Biashara ya Kadi Benki ya NMB, Philbert Casmir (katikati),
akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale
Zanzibar, Dk. Amina Ameir Issa, mfumo wa malipo wa Lipa Mkononi (QR)
kwa ajili ya wizara hiyo. Kushoto ni Meneja Biashara NMB Zanzibar -
Naima Said Shame.
Friday, July 15, 2022

NMB yakabidhi mashine za Malipo kwa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment