Mkurugenzi
wa Lake Oil Group, Ally Edha Awadh mara baada ya kupokea Tuzo ya
Mfanyabiashara Kijana kwa mwaka 2022 katika bara la Afrika.
***************************
Mkurugenzi wa Lake Oil Group, Ally Edha Awadh jana amepokea Tuzo ya Mfanyabiashara Kijana kwa mwaka 2022 kwa Afrika nzima.
Tuzo
hiyo alipokea jana nchini London, Uingereza baada ya kuwashinda
wapinzani wake watatu, Sangu Delle, ambaye ni Mwenyekiti wa kampuni ya
Golden Palm Investments Corporation ya nchini Ghana.
Wengine ni
Stephen Sembuya, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Pink Foods
Industries ya Uganda na Emmanuel Ademola Ayilara, Mtendaji Mkuu wa
kampuni ya LandWey Investment Limited ya nchini Nigeria.
Awadh
ambaye ni Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo iliyojikita kweye biashara ya
mafuta na gesi, amekabidhiwa tuzo hiyo Jana kwenye Ukumbi wa House of
Lords jijini London, Uingereza ambazo ni miongoni mwa kumbi maarufu
zaidi duniani.Tuzo hizo zinazotolewa na Jarida la African Leadership.
Lake
Oil imejikita zaidi katika biashara ya vituo vya kuuza mafuta kwenye
maeneo mbalimbali nchini sambamba na gesi zinazotumika kwa matumizi ya
nyumbani.
Mbali na hilo, Awadh anatajwa kama mfano kwa vijana
ambapo, kupitia kampuni zake hizo amesaidia kutoa ajira kwa makundi ya
vijana huku ufanisi wa kampuni hizo ukichukuliwa kama mfano bora kwa
vijana kuendesha biashara kwa tija.
Akizungumza mara baada ya
kukabidhiwa tuzo hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Lake Oil alisema ilikuwa
kumbukumbu ambayo hataisahau kwa maisha yake yote.
“Nilikabidhiwa
Tuzo ya Kiongozi wa Biashara Vijana barani Afrika katika Jumba la
Mabwana Mashuhuri hapa London, mbali ya faraja kwangu lakini nimefurahi
zaidi tuzo hii kupatikana kwa kijana wa Kitanzania,” alisema Bw.Awadh.
“Natoa
shukrani zangu za dhati kwa Mama na Baba yangu kwa Sala na Baraka zao
zisizo na mwisho, familia yangu, haswa Mke wangu, kwa nyakati zote
ambazo nimekuwa mbali na kuzingatia biashara zetu,” alisema Awadhi.
Pia
alitoa shukrani kwa timu nzima ya wafanyakazi wa makampuni ya Lake Oil
sehemu mbalimbali Afrika zilipo ofisi zake na mwisho kwa Mwenyezi Mungu
kwa kuwapa nguvu za kufanya kazi na kutimiza malengo yao.
Edha
ambae miaka ishirini na miwili (22) iliyopita aliweza kupata mapato yake
mwenyewe akifanya kazi kwenye mgahawa wa Mac Donald wakati akisoma
shahada yake yake ya kwanza huko Canada.
Aliporudi nchini kutoka
masomoni alianza ujasiliamali kuanzisha biashara yake ya kwanza ya kuuza
mitumba kutoka Canada hadi Tanzania. Nilijijengea mtaji na kuanzisha
tawi la kuagiza lori zilizofanyiwa ukarabati kutoka Uingereza hadi
Tanzania.
“Muda si muda nilikuwa milionea kijana nikiwa na umri
wa miaka 26 tu.Nilifurahishwa sana nilipoenda kwa Wakala wa Ununuzi wa
Mafuta kwa Pamoja nchini Tanzania nikiwa na Ofisi yangu ya Biashara ili
kupata leseni ya Uagizaji wa Petroli” Alisema Bw. Awadhi akitoa ushuhuda
wake mbele ya wafanyabishara wenzake.
Alitimiliza mahitaji yote
ambayo yalimwezesha kuwa kati ya wafanyabiashara wakuu. Ilikuwa mwaka
2006 ambapo Lake Oil ilizaliwa na baada ya kupata leseni iliyobaki
imekuwa historia nzuri kwake na pia kwa nchi yake Tanzania.
Tangu
wakati huo nimeongeza biashara yangu sio katika mafuta pekee bali hata
katika uwekezaji wa viwanda. Pia nimeendelea kuwekeza katika nchi
nyingine na kuacha alama katika nchi hizo kama muwekezaji kutoka
Tanzania.
Aliwaomba washiriki wa tuzo hiyo, wasiruhusu hadithi
yake nzuri ya mafanikio iwadanganye, wamekumbana na changamoto kadhaa
kwa miaka mingi, ikiwa ni pamoja na Kimbunga Idai ambacho kilikumba na
kuteketeza ghala kubwa ya kuhifadhia mafuta alioijenga nchini Msumbiji
mwaka wa 2019.
Baada ya miezi 9 moto ulizuka katika Ghala ya
kuhifadhia mafuta lake Oil makao makuu kigamboni Dar es Salaam na
kusababisha uharibifu na hasara kubwa. Sekta yetu ni tete na kwa haraka
mabilioni yanaweza kupotea.
Janga la Covid-19 ilitufunza
ustahimilivu mkubwa katika biashara. Tulijifunza, hata bidhaa ya thamani
kubwa haina thamani wakati hakuna Mahitaji. Hata hivyo, ujumbe wangu
hapa ni kwamba unaweza kupitia kila aina ya vikwazo maishani.
“Muhimu
ni kuvumilia na usikate tamaa. Kuna suluhu daima na kila mara kuna
mipango A au B na hata C, Nimejifunza kamwe kutokua na hofu ya kufikiri
na hata kutoka nje ya boksi”.Alimalizia Bw.Awadh. Mungu ibariki Afrika;
Mungu ibariki Tanzania na Mungu ibariki Lake Group.
Tuesday, July 5, 2022

MKURUGENZI LAKE OIL APOKEA TUZO YA MFANYABISHARA KIJANA AFRIKA NCHINI UINGEREZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment