

BALOZI Maimuna Tarishi, Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Umoja wa Mataifa, Geneva alimpongeza Bi. Michelle Bachelet kufuatia kumaliza kwa muda wake katika nafasi aliyokuwa akihudumu ya Kamishna Mkuu wa Baraza la Haki za Binadamu.
Aidha, Mhe. Balozi alitumia fursa hiyo kumpatia wasilisho lenye
ufafanuzi kuhusu Pori Tengefu la Loliondo na hifadhi ya Ngorongoro, na kuhimiza Jumuiya ya Kimataifa kuepuka kuamini taarifa za upotoshwaji zinazoenezwa kuhusu maeneo hayo; na kuwa hakuna mkazi yoyote aneyeondolewa kwa nguvu kama inavyodaiwa.
Alihitimisha kwa kumhakikishia Bi. Bachellet kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendeleza ushirikiano na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na kumtakia kila la kheri katika majukumuu yake.
No comments:
Post a Comment