- ASEMA HAKUNA SULTANI WALA MTU WA KUMTISHA MWENZAKE
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
MAKAMU
Mwenyezi wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu
Abdulrahman Kinana amewahimiza Wananchi hasa wanawake na vijana
kujitokeza na kuchukua fomu kuwania nafasi za uongozi wa ndani ya Chama
hicho na watakaochukua fomu haki itatendeka na hakuna wa kumtisha
mwenzake.
Akizungumza leo Julai 25,2022 baada ya kuzindua Mradi
wa fremu za maduka 15 zilizojengwa kwenye eneo la Ofisi za CCM Mkoa wa
Katavi,Kinana pamoja na mambo na mengine ameelezea mchakato wa uchgauzi
wa ndani wa Chama hicho unavyoendelea ambapo amewahimiza wanawake na
vijana kuchukua fomu kigombea nafasi za uongozi.
"Niwaombe akina
mama mkachukie fomu za kuwania nafasi za uongozi CCM, msiogope nendeni
mkachue fomu mpambane na wanaume.Pia nataka niwasihi vijana gombeeni
hizo nafasi, Uchaguzi ukija nafasi zitakuwa wazi na kila mtu anahaki
sawa na mwenzake.
"Hakuna masultani wa kukaa madarakani
milele,tuna uchaguzi kila baada ya miaka mitano, wenye kuwachagua Wana
CCM ,wana CCM wakikupenda ,wakikuheshimu na wakithamini mchango wako
watakupa kura lakini wasipothamini watakunyima kura.
"Nafikiri na
ninyi mnawafahamu wajumbe sio watu wazuri ,wajumbe hao wanaweza
kukwambia usiwe na wasiwasi tutakupa kura, halafu baadae unatoka kapa,
hivyo niwaombe sana vijana gombeeni ,kina mama gombeeni,tutatenda
haki,hatutampendelea mtu.
"Wala mtu asimtishe mwenzake kwamba
ukienda kuchukua fomu unaambiwa na wewe unatafuta nini,kwani na wewe
ulivyochukua si mwingine alikuwepo kabla yako, ndio umechukua nafasi
yake na mimi nakuja kukung'oa wewe,"amesema Kinana.
Wakati
Kinana akiyaeleza hayo Wana CCM na wananchi waliokuwa eneo hilo la Ofisi
za CCM Mkoa walionekana kufurahia kwa kupiga makofi na vigele.Kwa
kukumbusha tu Chama hicho kwa sasa kinaendelea na Uchaguzi wake wa ndani
na wanaCCM wameendelea kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali.
Awali
akipokea taarifa kuhusu ujenzi wa fremu hozo Katibu wa CCM Mkoa wa
Katavi Omari Mtuwa amesema ujenzi wa fremu hizo umegharimu Sh.milioni 65
na waliokodisha fremu hizo kwa mwezi watakuwa wanalipa Kodi
Sh.100,000."Tumeingia mkataba na waliojenga fremu hizi na leo tunafurahi
Makamu wa CCM Tanzania Bara Abdulrhaman Kinana umezindua.
Kinana
ambaye ameongozana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka
Hamdu Shaka amewasili mkoani Katavi leo na akiwa katika Mkoa huo pamoja
na mambo mengine amekaguaa miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya
utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana
akisalimiana na Wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Katavi baada ya kuwasili
katika wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi kwa ajili ya kukagua na kuweka
jiwe la Msingi kituo cha Afya cha Itenka.PICHA NA MICHUZI JR-KATAVI
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana
akizungumza jambo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu
Shaka akiwa katika matembezi na viongozi wa CCM na Serikali Mkoa wa
Katavi alipokuwa akikagua ujenzi wa fremu 118 zilizopo Mpanda mjini
mkoani Katavi.
Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana
akichota udongo kuweka kwenye mti alioupanda nje ya Ofisi za CCM Mkoa
wa Katavi ikiwa ni ishara ya kufika kwake katika ofisi hizo baada ya
kuzindua mradi wa fremu 15 za maduka ya biashara.Wengine wanaoshuhudia
ni viongozi wa ngazi mbalimbali wa Chama na Serikali katika mkoa huo.
Baadhi
ya Wanachama wa CCM na Wananchi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akizindua fremu 15 za maduka
yaliyojengwa katika majengo ya Ofisi za CCM mjini MPanda mkoani Katavi
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Abdulrhaman Kinana
akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi mradi wa fremu 15 za maduka ya
biashara zilizojengwa katika eneo la ofisi za CCM,Mpanda Mkoani
Katavi.Kinana amezindua mradi huo leo Julai 25,2022 baada ya kuwasili
mkoani Katavi kwa ziara ya kikazi sambamba na kukagua miradi ya
maendeleo.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa fremu 15 za maduka ya
biashara yaliyojengwa katika Ofisi za CCM Mpanda mjini Mkoa wa
Katavi.Wengine wanaoshuhudia ni viongozi wa Chama na Serikali mkoa huo
pamoja na wananchi
No comments:
Post a Comment