HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 26, 2022

KAMATI YA SENSA MKOA WA SINGIDA YAWATEMBEA WAKUFUNZI 216 WATAKAO HITIMU MAFUNZO KESHO

Na Dotto Mwaibale, Singida

WAJUMBE wa Kamati ya Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Singida wamewatembea Wakufunzi 216  watakao hitimu mafunzo yao kesho Julai 26, 2022 ambao watakwenda kutoa mafunzo kwa makarani wa sensa katika halmashauri zote mkoani Singida.

Wakufunzi hao walianza mafunzo hayo Julai 6, mwaka huu na kesho watayahitimisha kwa kuhutubiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge ambaye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi

Akizungumzia mafunzo hayo  Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida, Naing'oya Kipuyo, alisema yalianza Julai 6 mwaka huu na kesho ndiyo yatafikia tamati ambapo wahitimu hao nao watakwenda kuyatoa kwa makarani wa sensa katika wilaya zote. 

Kipuyo alisema Mkoa wa Singida unatarajiwa kuwa na makalani na wakufunzi wa sensa 5,402 ambao usahili wao ulifanyika kuanzia ulai 19, mwaka huu.

Alisema umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni pamoja na kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa;

Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali.


 Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida, Naing'oya Kipuyo, akizungumza wakati Wajumbe wa Kamati ya Sensa ya Watu na Makazi mkoani hapa walipowatembelea leo Julai 25, 2922 Wakufunzi wa Makarani wa Sensa wanaotarajiwa kuhitimu kesho Julai 26, 2022 katika ukumbi wa VETA mjini hapa ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge anarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Mjumbe wa kamati hiyo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Lucas Mwakatundu akijitambulisha kwa wakufunzi hao.
Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Dini mbalimbali mkoani hapa, Hamisi Kisuke akijitambulisha kwa wakufunzi hao.
Wakufunzi hao wakiwa wamesimama kuashiria kutoa heshima kwa wajumbe hao walipokuwa wakiingia ukumbini.
Washiriki wa mafunzo hayo ya ukufunzi wakiwa ukumbini.
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa ukumbini.
Wakufunzi hao wakiwa ukumbini.
Wahitimu wakionesha furaha yao ya kuhitimu mafunzo hayo

 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad