HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 13, 2022

Dkt. Stergomena Atembelea Mradi Ujenzi Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa

 



WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa eneo la Kikombo, wilaya ya Chamwino Dodoma tarehe 12 Julai, 2022.

Hii ni ziara ya pili kwa Mheshimwa Waziri kutembelea mradi wa ujenzi. Lengo la ziara hiyo, ni kukagua na kujionea hatua za maendeleo ya ujenzi unaotekelezwa kwa Force Account kwa kutumia wataalamu wa ndani. Mpaka sasa ujenzi wa mardi huo,. Ziara ya kwanza kya Mheshimiwa Waziri kutembelea ujenzi huo ilikuwa ni tarehe 28 Septemba, 2021.

Baada ya kutembelea na kupatiwa Maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Mheshimiwa Dkt. Stergomena amepongeza na kusifu kazi kubwa na nzuri inayoendelea kufanywa na kikosi kazi hicho, kwani ujenzi huo umefikia hatua nzuri “ kama ilivyoelezwa katika maelezo ya awali, hii ni mara yangu ya pili, nilipokuja na nilipokuja leo nimeona mabadiliko makubwa sana. Naomba nianze kwa kutoa pongezi kubwa kwa kazi kubwa inayoendelea kufanywa, maana hapa tulipofikia, tumefika mahali pazuri sana. Hii inathibitisha kuwa wanajeshi wanaweza kila kazi, na hakuna kazi inayoweza kufanywa na mwanajeshi ikashindikana”, alisema.

Akitoa maelezo ya utangulizi kwa Mheshimiwa Waziri, Msimamizi Mkuu wa mradi huo, Meja Jenerali Hawa Kodi amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo, umeanza tangu tarehe 20 Machi, 2020 na unatarajiwa kukamilika ifikakapo tarehe 22 Oktoba, 2022 ambapo umefikia asilimia 92. Utapokamilika utakuwa umegharimu takriban Shilingi 58.5 Iwapo ungetekelezwa na Mkandarasi kutoka nje ungegharimu takriban shilingi bilioni 127.19 na kuokoa zaidi ya Shilingi bilioni 68.7

Naye Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya mradi kabla ya Mheshimiwa Dkt. Stergomena kutembelea na kukagua jengo na kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika ujenzi huo. Amesema kuwa Makao Makuu hayo kwa pamoja yatakuwa na ofisi 1032 na yamegawanyika katika maeneo Makuu matatu ambapo eneo la Kwanza litakuwa na ofisi za Wizara ya Ulinzi na JKT kwa upande wa magharibi, eneo la Pili litakuwa na Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi upande wa mashariki na eneo la Tatu litakuwa na ofisi za Wakuu wa Kamandi chini ya JWTZ kwa upande wa nyuma.

Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa ulizinduliwa kwa kuwekewa jiwe la msingi na aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano na Amiri Jeshi Mkuu, Hayati John Pombe Joseph Maguli tarehe 25 Novemba, 2019 ambapo alitoa shilingi Bilioni 10 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad