HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 3, 2022

CCM Babati, Mambo yashaanza kupamba moto nafasi mbalimbali za Uongozi

 Na John Walter-Babati

Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama cha Mapinduzi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Babati Mjini, Baraka Mipiko wakati akizungumzia zoezi utoaji fomu za kugombea nafasi hizo ambazo zimeanza kutolewa Julai 2, hadi Julai 10 mwaka huu.

Aliwataka vijana wenye sifa wajitokeze kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi huo ili kuweza kuonyesha uwezo wao wa kuongoza.
“Kwa kasi ya Serikali ya sasa, inahitaji nguvu kazi ya vijana hivyo niwaombe vijana wajitokeze katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Mapinduzi ili kuweza kupata fursa ya kutumikia chama kwa kasi zaidi,” alisema Mipiko.

Miongoni mwa waliochukua fomu za kugombea ni pamoja na Wana Habari, Charles Mangwe aliyegombea nafasi ya Mjumbe mkutano mkuu Uvccm Mkoa na Mjumbe mkutano mkuu Ccm Wilaya (Babati Vijijini) na Elias Ernest (Babati Mjini), Katibu wa hamasa UVCCM Babati mjini Idd Sulle, Emanuel Khambay na wengine.

Katibu huyo wa UVCCM alizitaja nafasi zinazogombewa kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya, Wajumbe wa Baraza la Vijana wilaya (nafasi 5), Mwakilishi vikao vya Halmashauri kuu ya CCM wilaya (Nafasi 1), Mwakilishi UWT kutoka vijana kwenda UWT, Mwakilishi kutoka Vijana kwenda wazazi pamoja na Wajumbe wa baraza ngazi ya wilaya (nafasi 5).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad