
Akizungumza
katika semina hiyo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary
Masanja (Mb) amesema Wizara yake haifurahishwi na matukio yanayotokana
na wanyama wakali na waharibifu.
“Hata
sisi wizara hatufurahishwi kuona wananchi wanateseka kutokana na
changamoto ya wanyama wakali na waharibifu kwa sababu wengine wanapoteza
maisha au kupata ulemavu.” Mhe. Masanja amesisitiza.
Aidha,
amesema Serikali ina mikakati mbalimbali ya kukabiliana na changamoto
hizo ikiwamo kuweka maboya katika maeneo ambayo wavuvi wanavua samaki
ili kuonyesha mipaka ya hifadhi na kuangalia namna ya kuboresha kifuta
jasho/machozi.
Mhe.
Masanja amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa
fedha za UVIKO 19 ambazo zitatumika kwa ajili ya kuchimba mabwawa ndani
ya hifadhi ili wanyama waweze kupata huduma ya maji na kuacha kuingia
katika makazi ya watu.
Naibu Waziri Masanja ameahidi kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment