HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 22, 2022

WAZIRI JAFO ARIDHISHWA MAENDELEO UJENZI WA JENGO LA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 22, 2022.

Akizungumza mara baada ya kukagua jengo hilo Dk. Jafo alionesha kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo akimtaka mkandarasi Kampuni ya SUMA JKT kuongeza kasi ya ujenzi ili likamilike na hatimaye lianze kutumika.

Dkt. Jafo aliishukuru Kampuni ya SUMA JKT ambayo imepewa kazi ya kutekeleza mradi huo kwa hatua iliyopiga pamoja na kamati iliyoteuliwa kuusimamia ujenzi huo. 

“Pamoja na kuwa mradi huu tunatakiwa tuukamilishe Novemba tisa mwakani ya miaka miwili lakini ikiwezekana hata ukamilike haraka zaidi na, ijapokuwa mkataba unasema kazi inaisha mwaka mmoja lakini ikiwezekana by mwanzoni mwa mwakani iwe imekamilka,” alisema Jafo.

Hata hivyo waziri huo alitoa maelekezo kwa wakandarasi wote wanaojenga majengo ya Serikali katika maeneo mbalimbali kuweka mfumo kuvunia maji ya mvua ili kunusuru athari za mafuriko pamona kuwa na hifadhi ya maji.

Awali akiwasilisha taarifa ya mradi huo Karani wa Mradi wa Ujenzi Bi. Philomena Bango alisema kazi mbalimbali zinaendelea kutekelezwa kulingana na mpango kazi (master program) uliowekwa.

Bi. Philomena aliongeza kwa kusema kuwa hadi kufikia sasa mkandarasi ameshakamilisha kazi ya ujenzi wa mradi kwa asilimia 33 na kuwa wana matumaini ya utakamilika kwa wakati.

Hata hivyo, alisema kuwa mkandarasi huyo anakabiliwa na changamoto ya kupanda kwa gharama za vifaa vya ujenzi vikiwemo ndondo.

Ofisi ya Makamu wa Rais ilisaini mkataba wa sh. bilioni 18.8 na Kampuni ya SUMA JKT wa kuanza ujenzi huo Oktoba 13, 2021 na kukabidhi rasmi eneo la ujenzi kwa Mkandarasi baada ya kushinda zabuni ambapo ujenzi wake unasimamiwa na Msimamizi Elekezi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa ziara ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 22, 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitoa maelezo wakati wa ziara ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 22, 2022.
Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais lililopo Mtumba jijini Dodoma ambalo liko katika hatua za ujenzi leo Juni 22, 2022 ambalo limekaguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo Juni 22, 2022.

(PICHA BA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad