HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 22, 2022

WATOTO WAWILI WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA TRENI, TABORA

 

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
WATOTO wawili kati ya watu wanne wamepoteza maisha katika ajali ya Treni iliyotolea mkoani Tabora, baada ya Treni hiyo ya abiria yenye namba Y 14 yenye injini namba 9019 iliyokuwa inasafiri kutoka mkoani Kigoma kuelekea Dar es Salaam kupata ajali katika eneo la Malolo, Tabora majira ya Saa 5 Asubuhi, Juni 22, 2022.

Taarifa za vifo hivyo zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano, Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamila Mbarouk huku akisema majeruhi 132 wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa, Kitete - Tabora kwa ajili ya matibabu na wanaendelea vizuri.

“Ajali imesababisha jumla ya vifo 4 wakiwemo Watoto 2, wakike mwenye umri wa miaka 5 na wakiume miezi 4 na watu wazima wawili, mwanaume na mwanamke”, ameeleza Jamila kupitia taarifa hiyo.

Amesema Shirika linaendelea na zoezi la kuwasafirisha manusura wa ajali kutoka mkoani Tabora ili kuendelea na safari ya kuelekea Dar es Salaam. Amesema Shirika linaendelea kufuatilia Kwa karibu, kufahamu chanzo cha ajali hiyo ili kuchukua hatua zaidi.

Treni hiyo iliondoka Stesheni ya Kigoma majira ya Saa 2 Usiku siku ya Jumanne tarehe 21, Juni 2022 kuelekea Dar es Salaam, ikiwa na Behewa 8 na Abiria 930 kabla ya kupata ajali katika eneo la Malolo.

Shirika la Reli nchini (TRC) imetoa pole kwa Familia za marehemu na linawaombea majeruhi wa ajali wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu ya ujenzi wa taifa.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad