HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 17, 2022

VIONGOZI JAMII YA WAMASAI SAME WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUWAPATIA MILIONI 500/- KUJENGA KITUO CHA AFYA

 

Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogoro(kulia) akisimikwa kwa kukabidhiwa fimbo kama ishara ya  kuwa Kiongozi Mkuu wa Leigwanani kwa kuwa ni kiongozi wa Wananchi Wilaya Same Kata ya Ruvu wilayani humo.Anayemsimika ni Leigwanani Mkuu Kiongozi wa jamii ya Wamasai Paulo Laizer ( Katika)

Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogoro akizungumza mbele ya jamii ya Wamasai wakati wa tukio Maalum la jamii hiyo kutoa salamu za shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kuwapelekea fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo Sh.milioni 500 za ujenzi wa kituo cha afya.

Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogoro(kushoto) akimsimika Nginaya Ndeipa kuwa Kiongozi wa Leigwanani Kata ya Ruvu wilayani humo.
MKuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogoro (Katika) akiwa na viongozi wa kimila wa jamii ya Wamasai.
Sehemu ya wanawake wa Jamii ya Wamasai wakiwa makini kufuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea



Na Mwandishi Wetu,Same
VIONGOZI wa jamii ya Wamasai Leigwanani wakiongozwana Leigwanani Mkuu Mussa Paulo Laizer wametoa salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kuwapatia Sh.milioni 500 za ujenzi wa kituo cha afya.

Kupatikana kwa fedha hizo za ujenzi wa kituo Cha afya kinakwenda kuondoa changamoto ya kufuata umbali wa kilometa 55 huduma za afya na wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu lakini Rais Samia anakwenda kuondoa adha hiyo.

Viongozi hao wametoa salamu hizo za shukrani kwa Rais Samia , kupitia Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Arusha Edward Mpogoro huku wakimuomba kufikisha salamu hizo kwa Rais.

Akizungumza wakati akitoa salamu hizo Leigwanani Laizer amesema Rais Samia ameendelea kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuwatumikia Watanzania wakiwemo na wao ambao mbali ya kupata fedha za ujenzi wa kituo cha afya,pia wametengewa fedha Sh .milioni 500 kwa ajili y kujenga barabara ya Muungano - Jitengeni kwa kiwango cha Changarawe.

Pia na kuanza upembuzi yakinifu ya Ujenzi wa Daraja litakalounganisha Wilaya za Same na Sumanjiro. Hivyo wamemuhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Same wao wataendelea kumuunga Mkono Rais Samia kwa kazi nzuri anazofanya kuleta maslahi mapana kwa wananchi

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Same Edward Mpogolo amesema kuwa moja ya sifa ya viongozi bora ni wale wanaojali shida za wananchi wanaowaongoza na Rais Samia ameonesha hayo kwa vitendo kwa kuwajali wale anaowaongoza.

Mpogolo amesema kuwa mmoja wa wanasiasa waliopata kuishi nchini India Mahtma Ghandi aliwahi kuelezea kwamba atahakikisha Wahindi anaowaongoza wakae kwenye viti kwanza naye atakuwa wa mwisho kuketi. Akiwa na maana atawatengenezea wananchi wake mazingira ya kuwa matajiri naye atakuwa wa mwisho kupata mali

Aidha alinukuu kitabu cha TANU na Raia kilichoandikwa na baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuhusu kisa cha Mzee Maganga ambaye aliunguliwa na nyumba na chakula hivyo baadhi ya viongozi walikwenda kumjulia hali huku bila msaada wowote lakini mmoja wao alimsaidia kwa chakula, malazi na mavazi na kusisitiza kuwa huyo anayejua shida za wenzake ndie kiongozi anayehitajika na watanzania.

Hivyo Mpogoro amesema shida za jamii ya Masai wa Ruvu wilayani Same iwe shida ya jamii ya Wamasai wote huku akieleza kwamba Mkuu wa Mkoa na Rais Samia Suluhu Hassan wameshafikishiwa shida zao zinazowakabili na punde baadhi ya shida hizo zitatatuliwa.

Amewahakikishia wananchi wa Ruvu kuwa kazi ya ujenzi wa daraja linalounganisha Same na Simanjro itakayosimamiwa na Wakala wa Ujenzi wa Barabara Vijijini (TARURA) itaanza mara moja kwa kushirikiana na wananchi. Pia barabara ya Muungano Jitengeni Katika bajeti ya mwaka huu imetengewa Sh milioni 500, hivyo itatengenezwa kuanzia Julai 2022.

Aidha barabara nyingine zitakazotengenezwa ni ile ya Same hadi Ruvu na kwamba Serikali ya Mkoa inafanya jitahada ya kumaliza tatizo la kukabiliana na Tembo waharabifu wa mazao

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad