Mamlaka
ya mapato Tanzania (TRA) imeikabidhi Jeshi la Magereza kontena mbili za
mbolea zenye thamani ya Shilingi Milioni 124 ambazo kimsingi
umepitiliza muda wa forodha wa kuhifadhiwa mahali hapo.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi shehena hiyo yenye jumla ya mifuko 1960 ya mbolea
hiyo aina ya YARA, Afisa Mfawidhi wa TRA katika Bandari Kavu ya 'Dar es
Salaam Inland Container Depot' (DICD) Swalehe Rajabu alisema hatua hiyo
ni utekelezaji wa mamlaka ya kisheria aliyopewa kamishna wa TRA.
Alisema
baada ya mzigo huo wenye jumla ya Kontena tano kukaa kwa Musa mrefu
mahali hapo, Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo Kidata akaamuru mbolea hiyo
kutolewa kwa taasisi mbalimbali zinazojihusisha na kilimo likiwemo Jeshi
la Magereza.
" Huu ni
utaratibu wa kawaida Kwa TRA pale inapotokea mzigo wowote kupitiliza
muda wa kukaa kwa sheria na taratibu za kiforodha, tunaamini kwa
kuwapatia magereza mbolea hii kutawaongezea uzalishaji na hivyo kuleta
tija kwa Taifa" alisema Rajabu
Akipokea
msaada huo kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Magereza nchini, Mkuu wa
Magereza Dar es Salaam ACP George Wambuva mbali na kuishukuru TRA kwa
msaada huo, alisema mbolea hiyo imekuja wakati muafaka ambao Jeshi hilo
linajiandaa na msimu wa kilimo.
"Tunashukuru
kwa msaada huu, ukweli sisi kama Jeshi la Magereza kilimo ni sehemu ya
majukumu yetu hivyo imani yetu itatusaidia katika kufanikisha shughuli
za kilimo na kukifanya kiwe na tija zaidi" alisema ACP Wambuva
Alisema
malengo baadaa ya kuipokea mbolea hiyo wataipeleka katika Magereza
ambazo shughuli za kilimo zinatekelezwa na kwamba kwa upande wao Dar es
Salaam imekuwa kama sehemu ya kupokelea mzigo huo.
Aidha
alisisitiza wanakwenda kuutumia msaada huo kwa dhumuni lililokusudiwa
kwa lengo la kuhakikisha wanaongeza tija katika uzalishaji wa mazao
mbalimbali nchini
No comments:
Post a Comment