HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 23, 2022

TCAA yatoa msaada wa vitabu kwa shule ya Sekondari Minazi Mirefu

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa msaada wa jumla ya vitabu 467 vya masomo mbalimbali kwa shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu ya Kata ya Kipawa jijini Dar es Salam, ikiwa ni sehemu ya kurudisha huduma kwa jamii (CSR) kwa jamii inayoizunguka.

Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari alisema ni utamaduni wa TCAA kurejesha sehemu kwa jamii, na kuongeza kuwa Mamlaka inajukumu la kudhibiti usafiri wa Anga nchini pamoja na kutoa huduma za uongozaji ndege. Pia Mamlaka inaunga mkono kwa vitendo juhudi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwenye upande wa elimu,

Mkurugenzi Johari ameongeza kuwa,TCAA imeona ipeleke vitabu ili wanafuzi wavisome hasa ikizingatia kuwa miongoni mwa wanafunzi hao ndio watakaokuwa marubani wabobezi, wahandisi na waongoza ndege wa baadae wanaohitajika kufanya kazi kwenye Mamlaka hiyo ili kuendelea kudhibiti ubora wa huduma zinazotolewa.

“Linawezekana kwa sisi kuingia kwenye sekta ya Usafiri wa Anga kwa siku za baadae turushe ndege , tuongoze ndege, tutengeneze ndege”Mkurugenzi Johari aliwasisitizia wanafunzi hao.

Akisoma risala Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aveline Chugulu alisema shule hiyo yenye wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tatu ilianzishwa mnano mwaka 2020 na ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa vitabu vya kufundishia.Na kuongeza kuwa kwa msaada huo sasa wameweza kupata vitabu 24 vya Kemia, Vitabu 55 vya Fizikia, vitabu 29 vya Hesabu, na vitabu 16 vya Historia.

Pia wamepata vitabu 41 vya Bailojia, vitabu 79 vya Kiswahili vitabu 26 vya Uraia, Vitabu 11 vya Jiografia na Vitabu 186 vya kiingereza.

Akitoa shukran kwa niaba ya wanafunzi wenzake Usiana Mshanga alisema wanaishukuru TCAA kwa kuipatia Shule yao msaada huo wakiamini vitabu hivyo vitakuwa kichocheo muhimu sana katika kuongeza ufaulu wao katika shele yao.

Akihitimisha zoezi hilo Afisa Elimu Sekondari kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Musa Ally licha ya kuishukuru TCAA ameziomba taasisi nyingine kuiga mfano wa TCAA kwa jinsi inavyojitoa kwa kuitikia wito wa shule yao kwnaa kushirikiana nao kwenye sekta ya elimu nchini.

Hii si mara ya kwanza kwa TCAA kutoa msaada wa namna hiyo kTIK eneo la elimu, kwani kwenye mwaka huu wa fesha wa 2021/2122 TCAA imeshatoa msaada mwingine wa shilingi milioni 8.8 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya Msingi Rada iliyopo mkoani Songwe, vitanda 26 kwa shule ya sekondari ya Azania, ilitoa pia shilingi Milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 10 ya vyoo kwa shule ya Msingi Mzambarauni ya jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S.Johari akikabidi  vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu wakati wa zoezi la kukabidhi msaada huo katika Shule hiyo iliyopo katika Wilaya ya Ilala ikiwa ni Sehemu ya kurudisha kwa Jamii. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA),Hamza S.Johari akizungumza na viongozi wa Elimu wa Wilaya, Kata, Walimu pamoja na wanafunzi wakati wa zoezi la kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 katika Shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu vilivyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ikiwa ni kurudhisha kwa Jamii.
Diwani wa Kata ya Kipawa Aidani Amosi Kwezi akizungumza na wanafunzi pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) wakati wa zoezi la kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 katika Shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu vilivyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ikiwa ni kurudhisha kwa Jamii.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu Aveline William Chugulu akiwasilisha taarifa ya ununuzi wa vitabu kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA),Hamza S.Johari, Afisa Elimu Sekondari jiji la Dar es Salaam, Mussa Ally, Diwani wa Kata ya Kipawa Aidani Amosi Kwezi  pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 katika Shule hiyo vilivyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Salome Mallamia akitoa utambulisho pamoja na ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo wakati wa zoezi la kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 katika Shule hiyo vilivyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ikiwa ni kurudhisha kwa Jamii.
Afisa Elimu Sekondari jiji la Dar es Salaam, Mussa Ally akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kutoa msaada wa vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 katika Shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu iliyopo kata ya Kipawa wilaya ya Ilala.
Shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu Usiana Mshanga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake mara baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kutoa msaada wa vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 katika Shule hiyo iliyopo kata ya Kipawa wilaya ya Ilala.
Baadhi ya wanafunzi Shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu  wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa zoezi la kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 katika Shule hiyo vilivyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) ikiwa ni kurudhisha kwa Jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA),Hamza S.Johari akiwa kwenye picha ya pamoja na  Afisa Elimu Sekondari jiji la Dar es Salaam , Mussa Ally, Diwani wa Kata ya Kipawa Aidani Amosi Kwezi  pamoja na walimu wa Sekondari ya Minazi Mirefu wakiongozwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimun Aveline William Chugulu mara baada ya kumalizika kwa zoezi kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 katika shule hiyo vilivyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S.Johari akiagana na wanafunzi Shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu iliyopo kata ya Kipawa wilaya ya Ilala mara baada ya kumalizika kwa zoezi kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 katika shule hiyo vilivyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA),Hamza S.Johari akiagana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu Aveline William Chugulu mara baada ya kumaliza zoezi kukabidhi msaada wa vitabu vya masomo tisa vipatavyo 467 katika shule hiyo vilivyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).
Baadhi ya vitabu vilivyonunuliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kwa ajili ya Shule ya Sekondari ya Minazi Mirefu
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad