HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 10, 2022

Target yatinga Mahakamani kusitisha kukamatwa gari zake

 

MKURUGENZI Mkuu wa kampuni ya uchimbaji visima ambayo inajihusisha kwenye miradi ya serikali Ravula (Target) Ravula Srinivasa Reddy amefungua maombi ya mapitio katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akipinga amri ya ukamatwaji magari yake matatu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Septemba 7, 2020.

Mwekezaji ambaye ni raia wa India ameomba amri hiyo ya zuio la muda dhidi ya wajibu maombi na mawakala au mtu yeyote anayefanya kazi kwa niaba yao kutokufanya lolote kuhusiana na magari hayo wakati akisubiri kusikilizwa na kuamuriwa kwa maombi yake hayo ya mapitio.

Mwekezaji huyo anadai kuwa amekuwa akifanyiwa Matukio yanayomkatisha tamaa ingawa anadai kuwa hana tatizo na Serikali huku akielekeza malalamiko yake kwa mahakama.

Anadai kuwa ameathirika sana kiuchumi kwa kukosa kipato kwani ameshindwa kuendelea na shughuli zake na kusababisha kushindwa kukamilisha miradi mbalimbali ya Serikali ya uchimbaji visima katika meneo mbalimbali nchini na hata kiafya kwani yamemsababisha maradhi.

magari matatu yaliyoamriwa kukamatwa ni T 392 BIJ zote aina yaTata, T476 DER aina ya Ashok na T 252 DKM aina ya AMW huku dalali aliyeelekezwa kufanya kazi hiyo akiwa ni Abdallah Makata wa Sensitive Auction Mart ambaye.

Septemba 23/2020 alisema Septemba 17,2020 alikamata magari manne huko Dodoma ambapo gari moja yenye namba za usajili T 394 DPB ambayo haikuwepo kwenye oda na kwamba magari hayo ni mali ya Escon Borewell Limited wakati si kweli ni mali ya Target Borewells Limited.

Awali mwaka 2012 Shabani Cosla alifungua kesi ya madai namba 99 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Kampuni Escon Borewell Co. Ltd akidai Sh 18,271,030 kama hasara iliyotokana na kuvunjika kwa mkataba wa kukodisha gari yake yenye namba za usajili T. 884 AKV aina ya Mitsubish Fuso.

Pia alidai Sh milioni nne kama gharama ya kuvuta gari hiyo kutoka Iringa kwenda Dar es Salaam, riba kwa kiwango cha kibiashara asilimia 20, riba kwa kiwango cha mahakama kufuatia hukumu, gharama za kesi na nafuu nyinginezo ambazo mahakama itaona kwamba zinafaa.

Escon Borewell Co. Ltd iliwakilishwa na wakili Thomas Massawe, lakini hakufika mahakamani hivyo kesi kusikilizwa upande mmoja.

Mahakama hiyo katika hukumu yake iliyotolewa na Hakimu Waliarwande Lema Juni 24, 2015 ilimpa ushindi Cosla na kumwamuru mdaiwa (Escon) kumlipa au kumrejeshea gari lake likiwa katika hali nzuri au pesa sawa na thamani ya sasa gari hilo.

Pia iliamuru alipwe fidia madhara ya jumla kwa hasara ya matumizi ya gari hilo kiasi cha Sh90 milioni; Sh20 milioni kama fidia ya adhabu, riba ya asilimia 9 kwa mwaka malipo ya fidia ya hasara ya jumla kwa kuvunja mkataba, mpaka siku ya hukumu.

Pia iliamuru alipwe riba ya asilimia 7.5 ya kwa mwaka kutoka tarehe ya hukumu mpaka kukamilisha malipo yote pamoja na gharama za kesi.

Hata hivyo wakili wa Target Emmanuel Safari anadai kuwa Shabani aliidanganya mahakama hiyo kuwa Fuso hiyo ni yake wakati TRA ilikuwa kwenye jina la Godfrey Yohana Gamariel na kwenye mkataba alioutoa kwenye kesi hiyo inaonesha Juni 2,2011 alimkodisha G. Ramakanka kwa malipo ya Sh 2.2 milioni huku akishuhudiwa na Rehema Salim. Hivyo Shabani katika hatua ya kufungua kesi alidanga mahakama kuhusu umiliki wa gari na mtu aliyemkodisha gari.

Pia alisema kuwa hata hivyo baada ya kufanyika mawasiliano na ofisi ya Wakala wa usajili wa biashara na leseni ‘Brela’ ilieleza hakuna Kampuni iliyosajiliwa kwa jina la Escon Borewell Co. Ltd hivyo kwa mujibu hayo hakuna wakurugenzi ,Anuani wala hisa).

Miezo sita baadaye baada ya hukumu hiyo, Januari 15, 2016 Cosla alifungua maombi ya kukazia hukumu dhidi ya kampuni ya Target Borewells Limited, aliomba alipwe Sh 380 milioni badala ya Sh110 milioni na bila kuonesha kiwango hicho cha Sh 380 milioni kilipatikanaje.

Katika maombi hayo ya kukazia hukumu, Cosla alidai kuwa mdaiwa alibadilisha jina kutoka Escon Borewell Co. Ltd kuwa SBJ Borewells na baadaye Target Borewells Limited na kwamba wakurugenzi nao wa Escon Borewell Co. Ltd wameenda SBJ Borewells na baadaye Target Borewells Limited wakati si kweli.

Kufuatia udanganyifu huo Mei 9,2016 mahakama ilitoa katika uamuzi ilitoa amri na hati ya ukamataji ikielekeza magari T 975 BMQ, T 346 CHC mali ya Target Borewells Limited na gari T344 CHC mali ya SBJ Borewells yakamatwe na dalali wa mahakama Charles Sengo wa kampuni ya CDJ Classic Group Ltd.

Dalali huyo alitekeleza amri hiyo na Septemba 13,2016 aliifahamisha mahakama kuwa ameyauza magari hayo katika mnada wa hadhara kwa Mariyam Nassoro Hamadi kwa jumla ya Sh 200 milioni.

Kampuni ya Target ilifungua maombi namba 186 ya mwaka 2016 dhidi ya Shaban Cosla, CDJ Classic Group Limited ikiiomba itoe amri ya kuondoa hati ya ukamataji gari namba T 975 BMQ na ichunguze uhalali ukamataji wa gari hilo.

Pia iliomba kutengua amri ya ukamataji dhidi ya gari hilo na kuachilia gari hilo, gharama za kesi na amri nyingine zozote ambazo mahakama itaona zinafaa.

Target ilidai kuwa gari hilo likamatwa kimakosa na mjibu maombi wa kwanza (Shaban), kupitia kwa dalali huyo kwa kusudi la utekelezaji wa tuzo (amri) Mahakama ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mahakama hiyo katika uamuzi wake uliotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Cyprian Mkeha, Mei 26, 2017 ilikubaliana na pingamizi la Target na kuamuru gari hilo liachiliwe huru na kurejeshwa kwa mwombaji (Target) huku ikiamuru aliyelinunua arejeshewe pesa zake.

Pia ilielekeza mjibu maombi wa kwanza ndio atawajibika kwa gharama alizozitumia mjibu maombi wa pili na gharma nyinginezo huku ikielekeza mjibu maombi wa kwanza atafute mali huru za mshindwa tuzo (Escon) au vyovyote kwa kufuata taratibu za kisheria kabla ya kukamata mali za mtu mwingine.

Hata hivyo Cosla hakukubaliana na uamuzi huo badala yake alifungua maombi ya mapitio Mahakama Kuu.

Aliiomba mahakama hiyo kuitisha kumbukumbu (za mwenendo wa shauri la Kisutu), kuchunguza na kupitia uamuzi wana mwenendo wa Mahakama ya Kisutu katika shauri la maombi namba 186 la mwaka 2016, ili kujiridhisha na usahihi, uhalali, utaratibu wa mwenendo uamuzi na amri ya Mei 26, 2017.

Pia aliiomba mahakama hiyo kugeuza, kutengua na kutupilia mbali mwenendo na uamuzi wan Mahakama ya Kisutu wa Mei 26, 2017, na kukubali tunzo yake katika kesi namba 99 ya mwaka 2012 kulipwa jumla ya Sh200 milioni zilizowekwa katika akaunti maalum ya Mahakama iliyoko Benki Kuu.

Gharama za shauri hilo (aliliolifungua yeye) na la Kisutu (alilopinga uamuzi wake) zibebwe na mjibu maombi wa kwanza (Target) na nafuu au amri nyinginezo ambazo mahakama itaona zinafaa.

Mahakama hiyo katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji John Mgetta, Februari 25, 2019 ilitengua uamuzi huo wa Mahakama ya Kisutu.

Ilitengua na kutupilia mbali mwenendo wote, uamuzi na amri za Mahakama ya Kisutu katika shauri la maombi namba 186 la mwaka 2016 na ikaamuru alipwe Sh200 milioni haraka iwezekanavyo na mjibu maombi wa kwanza kulipa gharama za shauri hilo la maombi.

Jaji Mgetta alitengua uamuzi huo akieleza kuwa mombi hayo yaliungwa mkono na kiapo ambacho hakikuwa halali, na kwamba mwombaji aliwasilisha kiapo kinzani nje ya muda aliopewa bil kueleza sababu za kuchelewa na pia kwamba mnunuzi wa gari hilo hakuunganishwa katika maombi hayo

Miaka minne baadaye Shabani alifungua maombi mengine ya utekelezaji akidai Sh 230 milioni na hakueleza ni za nini huku akidai wakurugenzi wa kampuni ya Escon Borewell Co. Ltd ni R. S. Reddy, Bal Reddy Sama, Janga Reddy Pakkiru, Baswa Reddy Manne na Mehul Madania wakati akijua si kweli.

Alijaza magari 11 akitaka kuyakamata ambayo ni T 171 AUP aina ya Nisan, T 578 BIJ na T 392 BIJ zote aina yaTata, T133 BYK aina ya Nisan, T474 DER na T476 DER zote aina ya ASHOK,T 720 DFV aina ya Toyota, T517 DKG aina ya Tata, T 252 DKM aina ya AMW, T874 DNC aina ya Nisan .

Hata hivyo kwenye samasi zilionyesha mdaiwa ni Escon Borewell Co. Ltd na muhuri uliogongwa kwenye samasi unaonesha ni Excon Borewell Services ikiwemo za Februari 5 /2014 na ya Februari 8/2016 hivyo inaonyesha samasi zilikuw zikipokelewa na mtu tofauti

Kufuatia udanganyifu huo Septemba 7,2020 mahakama ya Kisutu ilitoa hati ya kukamata mali yaani magari matatu matatu yakamatwe ni T 392 BIJ zote aina yaTata, T476 DER aina ya Ashok na T 252 DKM aina ya AMW na dalali aliyeelekezwa kufanya kazi hiyo ni Abdallah Makata wa Sensitive Auction Mart ambaye Septemba 23/2020 alisema Septemba 17,2020 alikamata magari manne huko Dodoma ambapo gari moja yenye namba za usajili T 394 DPB ambayo haikuwepo kwenye oda na kwamba magari hayo ni mali ya Escon Borewell Limited wakati si kweli ni mali ya Target Borewells Limited.

Ingawa magari hayo yalidaiwa kununuliwa na Mariam Nassoro Hamad, lakini Marima katika maelezo yake aliyoyatoa Polisi japo amekiri kuwa Shanan ni kaka yake lakini amekana kununua magari hayo wala kuhusika na lolote katika kesi hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad