HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 24, 2022

TAMWA-ZNZ yatangaza awamu ya pili Tuzo za wanahabri Z’bar

 

Sehemu ya waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali Zanzibar wakisiliza taarifa ya utolewaji wa awamu ya pili ya tunzo ya takwimu na habari zinazowahusu viongozi wanawake.CHAMA cha Waandishi wa habari TAMWA-ZNZ kimesema jitihada zaidi zinahitajika ili kuleta mabadiliko ya baadhi ya sheria ,sera, na mifumo iliyopo ambayo inaonekana bado inamnyima fursa mwanamke za kushika nafasi za uongozi ili kuhakikisha usawa wa jinsia unazingatiwa kwa kuteuliwa au kuchaguliwa kwa upande wanafasi za kiutawala na kisiasa.


Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Chama hicho wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja katika mkutano maalumu ulilenga kuzinduliwa kwa awamu ya pili ya tunzo za waandishi wa habari kuhusu wanawake na uongozi pamoja natakwimu.

Alisema pamoja na jitihada na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kuridhia mikataba ya kitaifa na kimataifa Pamoja na malengo endelevu ya milenia na ASASI za kiraia zinazojihusisha na utetezi wa haki za wanawake katika kuwajengea uwezo na kuwahamasisha kugombea nafasi mbalimbali.

Alisema bado takwimu zinaonesha kuwa ipo namba ndogo ya viongozi wanawake katika ngazi mbali mbali ukilinganisha na wanaume katika nafasi za kiutawala lakini Zaidi kwenye nafasi za kisiasa ambako bado kunaonekana mwanamke anakosa fursa hasa katika nafasi za juu zakushika uongozi katika miundo ya vyama vya siasa vyenyewe Pamoja na kuwa na jumuiya za wanawake katika vyama hivyo

Alieleza kuwa hadi sasa takwimu zinaonesha ni mawizi 6 tu wanamwake kwenye idadi ya mawaziri 18 ambapo ni sawa 33.3 % vile vile katika nafasi za ma naibu mawaziri ambapo hadi sasa ni 1 kwenye idadi ya manaibu Waziri 7 ambapo ni sawa na 14.3 %, hali hii pia inaonekana katika nafasi za makatibu wakuu wakuu 5 tu kati 12 ambao ni wanaume sawa na 29.4 % samba na wakuu wa mikoa ni 1 tu ndio mwana mke kati ya 5 hali hii pia imejitokeza pia katika ngazi za halmashauri na serikali za mitaa wawilaya kwenye viongozi wa shehia

Sambamba na hayo Mkurugenzi huyo alisema Chama cha waandishi wahabari waanawake Tanzania ofisi ya Zanzibar (TAMWA), ikishirikana na Jumuiya wanasheria wanawake (ZAFELA) na jumiya ya Utetezi wa jinsia na mazingira Pemba (PEGAO) kupitia udhamini wa Ubalozi wa Norwey nchini Tanzania inatekeleza mradi wa kuwainua wanawake katika Uongozi (SWIL).

Aidha alisema kupitia mradi huu wa kuwawezesha wanawake katika uongozi kwa kiasi kikubwa imeweza kulipa umakini wa karibu Zaidi , fursa uwezo, mapungufu juu ya jitihada kufikia kutambua usawa wa kijinsia na uwewezashaji wa wanawake hususan katika nafasi za uongozi .

Hata hivyo kwa upande wa vyama vya siasa , baadhi ya vyama vimekuwa vikibana fursa kwa wanawake kuwapa nafasi za juu kuongoza kutokana na mifumo waliyonayo au kutokuwa na mikakati ya makusudi kwa kulizingatia suala la usawa wa jinsia katika nafasi za uongozi

Hivyo basi Pamoja na kuendesha shughuli mbalimbali kupitia mradi huu TAMWA-ZNZ mwaka 2021 iliandaa mashindano ya uandishi mahiri juu ya kuripoti tawimu zinazohusiana na ushirikishwaji wa wanawake katika nafasi za uongozi Zanzibar.

Lengo kuu La mashindano haya ni kushajiisha waandishi wa Habari kuandika Habari za umahiri ili kuhakikisha tauluma ya umahiri Pamoja na mwamko katika fani ya Habari kwa kuzingatia utambuzi wa vyombo vya Habari wenyewe juu ya dhamira ya TAMWA katika kutetea haki za wanawake na Watoto kwa kufanya shughuli za kuengeza uwelewa ikiwemo matumizi ya vyombo vya Habari kupitia magazeti, televisheni, redio na mitandao ya kijamii.

Akifafanua Zaidi alisema katika zoezi hilo lilifanikiwa kuibua na kuwapata washindi ambao ni waandishi katika vyombo mbali mbali walioshinda kutokana na kazi zao zilizoshindanishwa zilizozingatia matumizi sahihi ya takwimu, pamoja na vigezo vyengine vya habari za umahiri Zanzibar kupitia uanzishwaji wa tunzo ya uandishi wa habari ya “Sauti Yangu, Haki Yangu” sambamba na kuwashajiisha wanahabari kuona umuhimu wa kuzingatia dhana hii katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wao katika jamii na kuwafikia makundi yaliyo pembezoni kuweza kupaza sauti zao kupitia vyombo vya Habari kwa kuzingatia haki na usawa kijinsia.

Katika muendelezo wa shuguli za mradi kwa mwaka huu TAMWA ZANZIBAR imekusudia kuendesha mashindano ya Habari zinazohusiana zinazohusiana na ushirikishwaji wa wanawake katika nafasi za uongozi Zanzibar na changamoto zinazokabili jamii katika kujenga jamii ambayo inaheshimu haki , heshima katika usawa wa jinsia kwa kuzingatia makundi mengine yanayoishi na mazingira magumu na wanaotaka kusaidiwa kupaza sauti zao.

Katika mashindano ya mwaka 2021 jumla ya kazi 452 zilipokelewa, ambapo kazi 73 zilikuwa makala za magazeti, kazi 3 zilikuwa makala (documentaries) za televisheni, makala 116 zilikuwa za redio na makala 260 zilikuwa za mitandao ya kijamii kutoka vyombo mbali mbali vya Unguja, na Pemba, na kutolewa tuzo kwa kila mshindi

Hata hivyo TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na Jumuiya wanasheria wanawake (ZAFELA) na jumiya ya Utetezi wa jinsia na mazingira Pemba (PEGAO) kupitia udhamini wa Ubalozi wa Norwey nchini Tanzania kupitia mradi wa SWIL inapenda kuwaalika na kuwataka ushiriki wao Waandishi wote kitaaluma na wa kujitolea ambao huandikia magazeti kutoka Unguja and Pemba ambao Habari zao wanachapisha katika magazeti na Habari za kieletroniki kwa kuzisambaza katika maeneo mbali mbali kwa kuwalenga wahusika.

Vile vile TAMWA inawasisitiza washiriki wote walioshiriki katika shindano lilopita ambao alama zao hazikutosha kutumia fursa hii kuandika tena habari za umahiri zenye dhumuni linalohusiana na wanawake na uongozi kipindi cha mwaka cha mashindano ya 2022 kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo.

Akieleza kuhusu vigenzo vitakavyotumika katika kuhakiki kazi za waandishi na watayarishaji wa vipindi hadi kupata washindi, mbali ya kuzingatia vigezo vya kitaaluma na uandishi wa habari zenye umahiri, vigezo kadhaa kama vifutavyo,Ubora wa kazi utakaowasilishwa utaangaliwa uweledi, umahiri wa uandishi,Upekee wa mada ,Umuhimu wa kuzingatia uwiano wa usawa wa jinsia,vyanzo vingi vya habari vilivyojitawanya pamoja na ushirikishaji wa wananchi na wadau(different sources)Ubunifu wa mada husika.

Mpangilio wa mada,Ufasaha na mtiririko wa lugha,Kuzingatia maadili ya uandishi wa habari,Uweledi wa matumizi ya takwimu,matokeo baada ya kutoka habari au kipindi hicho (impact) Kipindi cha Redio na Televisheni kisichozidi dakika 30 na kuzingatia ubora wa sauti na ubora wa picha.

Katika mashindano ya mwaka 2021 jumla ya Habari 452 zilikusanywa kutoka vyombo mbali mbali vya Unguja, na Pemba, Habari hizi ni kutoka magazeti ,radio, televisheni na mitandao ya kijamii na kutolewa tuzo kwa kila mshindi

Mradi wa kushajiisha ushiriki wa wanawake katika uongozi na demokrasia ni mradi wa miaka minne (2020 – 2023), wenye lengo la kukuza ushiriki wa wanawake katika uongozi ambao unatekelezwa na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) jumiya ya Utetezi wa jinsia na mazingira Pemba (PEGAO) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway chini Tanzania.
Mkurugenzi wa TAMWA-ZNZ Dkt,Mzuri Issa akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari kuhusu awamu ya pili ya tunzo hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad