HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 23, 2022

TAASISI YA RUGE MUTAHABA KUZINDULIWA JUMAPILI

 Na Khadija Kalili

TAASISI ya Ruge Mutahaba inatarajiwa kuzinduliwa Juni 26, 2022 (Jumapili ijayo) ambapo taasisi hiyo imeanzishwa ikiwa ni baada ya miaka mitatu tangu alipofariki dunia ambapo lengo lake kubwa kuendeleza maono aliyokuwa nayo katika enzi za uhai wake ambapo alijikita zaidi katika ustawi wa vijana, wanawake na Tanzania nzima kwa ujumla.

Akizungumza kwa niaba ya familia Rwebu Mutahaba alipozungumza na Waandishi wa Habari Leo asubuhi katika Mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Regency Jijini Dar sea Salaam, alisema kuwa Taasisi hiyo ya Ruge Foundation imejikita katika dhima kuu Tano ambazo ni ubunifu, uvumbuzi, umahiri, upambanaji na uzalendo hivyo taasisi itashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, sekta binafsi na mashirika ya ndani na ya Kimataifa katika kuendesha miradi kwenye sekta mbalimbali Ili kutatua changamoto za wanawake na vijana hasa katika eneo la ajira na kutengeneza kipato.

"Enzi za uhai wake Ruge alijitahidi sana kuwekeza katika ubunifu na ujasiriamali wa vijana na wanawake ili kuwasaidia katika kuinua kipato, kuanzishwa kwa taasisi hii ni muitikio wa sauti za wananchi kutokana na nafasi kubwa aliyokuwa nayo Ruge katika kuwakilisha na kutekeleza maono yake chanya ya kimaendeleo yaliyolenga vijana na wanawake kwa kupitia miradi mbalimbali kama (Fursa)" alisema Rwebu Mutahaba.

Rwebu aliongeza kwa kusema kuwa Taasisi hiyo imekuja na mikakati wa kuendesha miradi ya kuwasaidia wanawake na vijana kwa kupitia ujasiriamali wenye tija , Sanaa na ubunifu.

Aliyataja maeneo yatakatopewa kibaumbele ni pamoja na ufadhili wa masomo na ushauri wa kitaaluma kwa vijana zaidi ya 5000 kwa mwaka, pia watawaunganisha vijana 10,000 na fursa za kiuchumi pamoja na kuitengeneza Kituo au sehemu ambayo vijana watakutana, kujadiliana changamoto wanazozipitia na kiunganishwa na wadau wezeshi alisema mmoja wa viongozi katika Taasisi hiyo Suma Mwaitenda.

Uzinduzi huo utarushwa moja kwa moja na vyombo mbalimbali vya habari nchini huku tukio hilo litakwenda hewani kuanzia saa tatu na robo usiku kupitia Clouds Tv, ITV, EATV na TVE.
Mwakilishi wa Familia ya Ruge Mutahaba, Bwana Rwebu Mutahaba amewaomba watanzania, vyombo vya habari na wadau wengine kushirikiana na Ruge Foundation kuendeleza maono ya marehemu Ruge Mutahaba ya kuinua vijana na wanawake kiuchumi.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa Clouds Media Group, Reuben Ndegi ambao ni washirika wa Ruge Foundation amesema wanajisikia vizuri kutoa mchango wako kama chombo cha habari kuendeleza mazuri ambayo aliyaacha Ruge Mutahaba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad